HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 25, 2016

AIRTEL YAKABIDHI MILIONI 20 NZEGA KUKOPESHA WANANCHI

Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (kushoto),  akikabidhi mfano wa hundi ya shilingi Milioni 20, kwa Mbunge wa jimbo la Nzega Mjini Mhe, Hussein Bashe.

xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kupitia mfuko wake maalum wa kusaidia jamii wa Airtel FURSA Tunakuwezesha leo imekabidhi hundi ya shilingi milioni 20 kwa Mbunge wa Nzega ikiwa ni harakari za kukamilisha dhamira yake ya kushirikiana na jamii katika kuinua vijana sehemu mbalimbali hapa nchini.

Akikabidhi hundi hiyo Mkurugenzi mkuu wa Airtel Bw Sunil Colasa alisema “Airtel imejipanga kwa kuhakikisha vijana wanaendelea kunufaika na mradi wa Airtel FURSA kwa kuwapatia misaada ya kukamilisha mipango yao waliyoipanga kwa kupunguza changamoto walizonazo ikiwemo ya ukosefu wa ajira na  mtaji ili watimize malengo yao katika biashara”

“Tunaamini kupitia ushirika wetu na Mbuge Nzega Mh, Hussen Bashe mfuko wa  Nzega Trust Fund utasaidia wananchi ndani ya vijiji 21 katika jimbo hilo ambapo malengo yetu ni kufanya mradi huu kuwa endelevu hata kwa majimbo mengine nchini” alisema Bw, Colasa

kwa upande wake Mbunge wa Nzega Mjini Mh, Hussen Bashe aliishukuru Airtel nakuahidi kusimamia mradi huo wa ukopeshaji kwa ajili ya kuweza kuinua vipato vya wananchi wa Nzega kama ilivyokusudiwa
“Nitoa wito kwa wananchi wote wenye malengo ya kujiendeleza kujitoza na kujisajili katia Mfuko wetu wa Nzega Trust Fund niliouanzisha kwaajili ya kuhakikisha tunaungana na wadau wenye nia ya kusaidia jamii kama Airtel FURSA ili kupunguza changamoto za maendeleo kwa wananchni hasa kwa  wanaokosa mitaji ya kuendesha Miradi yao mbalimbali”

“Airtel tayari wamezikabidhi pesa hizi kwangu ambazo tutazikopesha kwenu kwa Riba ya 1.5% pale unaporejesha na faida inayopatikana bado itaendelea kuwasaidia vijana wengine watakaotaka kukopa” Alieleza Mh Bashe
Mradi wa Airtel Fursa umeanzishwa Mei mwaka uliopita na tayari umewafikia vijana zaidi ya Elfu tano kutoka katika mikoa kumi nchini ikiwa ni pamoja na vijana zaidi ya 100 waliowezeshwa kwa kupewa mitaji na vitendea kazi  mbalimbali

Programu hii kati ya Airtel na Nzega Trust Fund chini ya Mbunge wa Jimbo la Nzega Mjini Mhe. Hussein Bashe, itawawezesha  zaidi ya  wajasiriamali 350 kunufaika na mikopo kupitia huduma ya Airtel Money.  Mikopo hii itatolewa kwa kikundi kilichoundwa na vijana watano ambao watapewa  mtaji kati ya shilingi  Shs.100,000 hadi 1,000,000  kulingana na mahitaji yao. Sambamba na mikopo ya  WanaNzengo Airtel FURSA vikundi vya wajasirilamali  vitaendelea kupewa mafunzo ya ujasiriamali ikiwa ni pamoja na  namna ya kuendesha vikundi pamoja na jinsi ya kutafuta soko.

No comments:

Post a Comment

Pages