Kaimu Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Kilimanjaro,Mawenzi Dkt Josephat Boniface akitoa maelzo mafupi kwa wafanyakazi wa Benki ya NMB tawi la Nelson Mandela waliofika hosptalini hapo kwa ajili ya kutoa zawadi kwa wagonjwa pamoja na msada wa vitendea kazi vya kufanyia usafi kwa hospitali ya Mawenzi.
Wafanakazi wa Benki ya NMB tawi la Nelson Mandela mjini Moshi wakishusha zawadi mbalimbali kwa ajili ya kugawa kwa wagonjwa waliolazwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Kilimanjaro,Mawenzi.
Meneja wa Benki ya NMB,tawi la Nelson Mandela ,Emanuel Kishosha akimueleza jambo Kaimu Mganga mfawidhi wa hospitai ya Rufaa ya mkoa wa Kilimanjaro,Mawenzi Dkt Josephat Boniface walipofika hospitalini hapo kutoa zawadi kwa wagonjwa waliolazwa.
Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro,Mawenzi Dkt Josephat Boniface akieleza changamoto mbalimbali zinazoikabili hospitali hiyo kwa wafanyakazi wa Benki ya NMB tawi la Nelson Mandela walipotembelea wagonjwa na kuwapa zawadi.
Meneja wa Benki ya Nmb tawi la Nelson Mandela mjini Moshi,Emanuel Kishosha akikabidhi msaada wa vitendea kazi kwa ajili ya usafi kwa kaimu mganga mfawidhi wa Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Kilimanjaro ,Mawenzi Dkt Josephat Boniface.
Wafanyakazi wa Benki ya NMB,tawi la Nelson Mandela wakiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa hosptali ya Rufaa ya Mawenzi.
Wafanyakazi wa Benki ya NMB,tawi la Nelson Mandela mjini Moshi wakiwa wamebeba vifaa mbalimbali kwa ajili ya kufanyia usafi katika hospitali ya rufaa ya Mawenzi.
Wafanyakazi wa Benki ya NMB,tawi la Nelson Mandela wakitoa zawadi mbalimbali zikiwemo Sabuni za kufulia,sabuni za kuogea ,dawa za meno,maji ya kunywa na vingine vingi kwa wagonjwa waliolazwa kati wodi mbalimbali hospitali ya rufaa ya mkoa ya Mawenzi. Kaimu Mganga Mfawidhi wa hosptali ya rufaa ya Mawenzi ,Dkt Josephat Boniface akifurahia jambo na mmoja wa wafanyakazi wa Benki ya nmb tawi la Nelson Mandela.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,Kanda ya Kaskazini.
No comments:
Post a Comment