Mkuu wa Wilaya ya Mbozi John Palingo akishukuru mara baada ya kupata msaada wa Cement1 kutoka benki ya Posta Tanzania (TPB). |
Mkuu wa Mkoa Songwe Picha ya Pamoja na Viongozi wa Mkoa wa Songwe na wadau mbalimbali. |
BENKI ya Posta
Tanzania(TPB) kupitia tawi lake Mkoani Mbeya, imetoa msaada wa mifuko ya
saruji 125 thamani ya shilingi milioni 2.5 kwa serikali ya Mkoa
mpya wa Songwe.
Akikabidhi mifuko hiyo ,
kwa uongozi wa serikali ya Mkoa wa Songwe, Meneja wa benki ya Posta mkoa wa
Mbeya, Humphrey Julius amesema benki hiyo iliguswa na suala la ujenzi wa
majengo mapya ya ofisi za Mkoa wa Songwe hivyo kuona umuhimu wa kuchangia ikiwa
kama faida wanayoipata kutoka kwa wateja wanaowahudumia.
Amesema, mbali na kutoa
msaada huo wa mifuko ya saruji, pia benki hiyo imeshakabidhi madwati 130
kwa baadhi ya shule za msingi za Wilaya ya Tunduma, Ileje zilizopo Mkoani
Songwe na dawati 30 kwa shule ya Mbeya Day Mkoani Mbeya.
Amesema, serikali pekee
haiwezi kufanya mambo yote ni lazima wadau zikiwemo Taasisi, Mashirika, Asasi
na mtu mmoja mmoja kuingiza mikono yao ili kuipungizia serikali mzigo.
Hata hivyo, akipokea
msaada huo, Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Luten Mstaafu Chiku Galawa, aliishukuru benki ya Posta kwa
msaada huo, muhimu kwani serikali ya Mkoinahitaji zaidi ya mifuko 50 elfu ya
saruji na mabati laki moja kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa majengo ya
ofisi pamoja na shule na Zahanati.
No comments:
Post a Comment