HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 12, 2016

MKUTANO WA WADAU WA NSSF KUFANYIKA JIJINI ARUSHA OKTOBA 20-21

WADAU wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) wanakaribishwa katika mkutano wa sita wa shirika hilo utakaofanyika Oktoba 20 na 21 katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa (AICC) Arusha.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Kaimu Mkurugenzi Uendeshaji, Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bathow Mmuni amesema kuwa maandalizi ya mkutano huo yanakaribia kumalizika kwahiyo  waajili na wadau wote wanaopenda kuhudhuria mkutano huo wanaombwa waendelee kujiandikisha katika Mtandaoni kupitia Tovuti ya www.nssf.or.tz. kabla ya Oktoba 18.

Amesema kuwa washiriki watatumiwa namba ya uandikishwaji kwenye Barua pepe zao (Email) namba hiyo itarahisisha utambuzi wa ushiriki wa mkutano huo,amesema kuwa  washiriki wa mkutano huo watajigharimia usafiri na malazi wawapo Arusha.
Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bathow Mmuni akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam,  kuhusu mkutano mkuu wa sita wa wadau wa NSSF uatakaofanyika jijini Arusha Oktoba 20-21. Kushoto ni Meneja Matekelezo wa NSSF,  James Oigo. (Picha na Francis Dande)

No comments:

Post a Comment

Pages