Mkuu wa Wilaya ya Chunya Rehema Madusa akimfariji Maria Solomoni ambaye alipoteza mtoto wake kwa uzembe wa muuguzi katika katika hospital ya Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya. |
Patricia Kisoti Muuguzi anayetuhumiwa kufanya uzembe uliosababisha Mama mjamzito kujifungua na mtoto wake kupoteza maisha katika hospital ya Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya. |
Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo ya Wilaya ya Chunya, Sasita Shabani akizungumza kuhusiana na tukio hilo la kufanyiwa ukatili kwa mama mjamzito na mmoja wa wauguzi. |
Wananchi na wanaopata huduma za afya katika Hospita ya Wilaya Chunya wakionesha nyuso za majonzi mara baada ya mmoja wa wananchi kufanyiwa vitendo vya kikatili. |
Jeshi la Polisi Wilayani Chunya Mkoani Mbeya linamshikilia muuguzi
wa afya katika hospitali ya Wilaya ya
Chunya, Patricia Kisoti, kwa kutokana na uzembe uliopekekea mama mjamzito
kujifungua mtoto akiwa amekufa.
Akizungumzia tukio la kukamatwa kwa muuguzi huyo Mwenyekiti wa
kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Chunya
Rehema Madusa amesema kitendo kilicho fanywa na muuguzi huyo nichakinyama
na kimetia aibu sekta ya afya.
Amesema September 4, mwaka huu katika hospitali ya Wilaya ya Chunya,
mjamzito huyo akiwa ameongozana na mwenzake walifika kituoni hapo usiku,
wakihitaji huduma ya haraka kutokana na hali ya mgonjwa kuwa mbaya.
Amesema licha ya mama huyo kufika akiwa katika hali mbaya
alijitahidi kujieleza ili apate huduma kwa waaguzi waliokuwa zamu akiwemo
mtuhumiwa huyo Patricia Kisoti ambaye ndiye aliyetakiwa kumhudumia mgonjwa huyo
lakini alishindwa kutoa ushirikiano badala yake alitoa majibu ya kejeli na
kushindwa msaada wowote.
Amesema kama mama huyo angemshughulikiwa kwa haraka ikiwa na
muuguzi huyo kutoa taarifa kwa ngazi za juu baada ya kuona tatizo hilo
haliwezi, basi mtoto huyo angekuwa hai.
Aidha, Mkuu huyo alimtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chunya,
Sophia Kumbuli kuhakikisha anachukua hatua za kinidhamu kwa wahusika wote.
Amesem kifo cha kichanga hicho, kwa asilimia kubwa kilitokana na uzembe wa muuguzi huyo kutokana
na maalezo yaliyotelewa mgonjwa huyo.
Akizungumzia sakata hilo, Maria Solomoni, amesema siku hiyo,
yeye akiwa ameongozana na mwenzake aliyemtambulisha kuwa alikuwa ni wifi yake,
walifika katika kituo hicho cha afya majira ya usiku, huku akiwa ameshikwa na
uchungu, ambapo waligonga mlango wa chumba cha nesi ambao kwa muda huo ulikuwa
umefungwa.
.
Maria, aliendelea kufafanua kuwa aliendelea kuteseka na mates
ohayo mpka majira ya saa kumi namoja alifajili ndipo alipoona wanaume wawili
wakimuhangaikia na kumuingiza katika chumba cha upasuaji na kufanyiwa
oparesheni.
Naye Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo ya Wilaya ya Chunya,
Sasita Shabani, alikiri kutokea kwa tukio hilo kituoni hapo na kwamba katika
uchunguzi wao wa awali umebaini kwamba katika tukio lililomkuta Maria Solomoni,
ndani yake kulikuwa na uzembe.
No comments:
Post a Comment