HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 04, 2016

NSSF YATOA MSAADA WA MIL. 50 UJENZI WA KITUO CHA POLISI


SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), limechangia  Sh. milioni 50 kusaidia ujenzi wa kituo cha Polisi Kiluvya Gogoni Wilaya ya Ubungo.


Akikabidhi hundi hiyo Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Prof. Godius Kahyarara alisema wameguswa na kituo hicho kutofanya kazi na kuamua kulisaidia jeshi la polisi kukijenga.

Kahyarara alisema msaada huo umetolewa kwa mujibu wa sera za shirika katika kusaidia jamii katika nyanja za Elimu, Afya, Mazingira, Michezo na maeneo mengine yaliyoainishwa katika sera.

"NSSF imeona ni vyema ishiriki katika suala zima lakuhifadhi na kulinda jamii na mali zao kwani jamii hiyohiyo ndio ambao shirika linategemea kulichangia na kisha kutoa mafao kwake kwa mujibu wa sheria za hifadhi ya jamii" alisema Kahyarara.

Mbali na kutoa msaada huo Kahyarara alisema lengo la kuimarisha ulimzi kwa maeneo yaliyo pembezoni mwa jiji shirika lao miaka michache iliyopiya imewezesha jeshi hilo katika ujenzi wa nyumba za Polisi kwa mikoa ya Dar es Salaam, Zanzibar na Pemba.

Hata hivyo aliwaomba watu wenye uwezo wajitokeze kuchangia ili kuweza kufanikisha ujenzi huo na kuimarisha ulinzi.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Simon Sirro, alisema kituo hicho kilivunjwa kwasababu kilikuwa kidogo na lengo la kujengwa ni ili kiwe kituo cha wilaya ya Ubungo.

"Nashukuru kwa msaada huu, fedha hizo ni nyingi tutazitumia kama zilivyokusudiwa, pia wadau wengine wajitokeze" alisema Sirro.
Kamanda wa Polis Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro akizungumza kabla ya kupokea msaada wa Sh. Milioni 50 kutoka NSSF kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa Kituo cha Polisi Kiluvya.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Godius Kayharara akizungumza kabla ya kukabidhi msaada wa Sh. Milioni 50 kwa Jeshi la Polisi kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa Kituo cha Polisi Kiluvya.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Godius Kayharara akimkabidhi hundi ya Sh. Mill. 50 Kamanda wa Polis Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa Kituo cha Polisi Kiluvya, katika hafla ilifanyika jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Godius Kayharara akimkabidhi hundi ya mfano ya Sh. Mill. 50 Kamanda wa Polis Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa Kituo cha Polisi Kiluvya, katika hafla ilifanyika jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Pages