HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 27, 2016

RAIA WA CHINA MBARONI DAR KWA UTEKAJI

Na Mwandishi Wetu

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema raia wa China wanaongoza kwa kuvunja sheria za nchi.

Kauli hiyo imetolewa jana jijini Dar es Salaam na Kamanda wa Polisi, Kamishna Simon Sirro ambapo raia hao wamekuwa hapa nchini kwa shughuli tofauti ikiwa ni pamoja na watalii na wawekezaji.

Alisema anawashikili raia wawili wa china, Wang Young Jing(37) na Chen Chung Bao(35) kwa kosa la utekaji nyara kwa mfanyakazi wa Grande Cassino Liu d o Hong (48).

Sirro alisema watekaji hao walivyomchukua mfanyakazi huyo walimpelea katika nyumba ya kulala wageni ya Palm Beach Hotel iliyoko upanga na kuanza kumpiga.

Alisema walipiga simu kwa wazazi wa mfanyakazi huyo wakidai watumiwe Yen 100,000 sawa na dola za kimarekani 19,000 na kwamba askari walivyofika eneo la tukio walimkuta Liu hajiwezi kutokana na kuvuja dam nyingi.

Katika tukio jingine Jeshi la polisi limekamata mtandao wa wezi wa magari ambapo kati yao ni mwanafunzi wa chuo cha CBE.

Alisema wanawashikilia watuhumiwa wanne kwa kosa la wizi wa magari ambapo walikutwa na gari namba T.290 DDM Toyota alphad.

Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Denis Ushak (25), Alfred Ditriki (33), Venance Bureta(23) pamoja na mwanafunzi huyo Valentino Godfrey.

Katika hatua nyingine jeshi hilo linawashikilia watu 57 kwa makosa tofauti ikiwemo panya road na uzururaji. Alisema Temeke walikamatwa watuhumiwa 21, Kinondoni 17 na Ilala 19

No comments:

Post a Comment

Pages