Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati ya
Utambulisho kutoka kwa Balozi mteule wa Ghana hapa nchini Kwame Asamoah
Tenkorang Ikulu jijini Dar es Salaam.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Mabalozi
waliowasilisha hati zao za utambulisho Ikulu Jijini Dar es Salaam ni Balozi wa
Jamhuri ya Sudan hapa nchini Mhe. Mahjoub Ahmed Abd Allah Sharfi, Balozi wa
Jamhuri ya Slovakia hapa nchini Mhe. Frantisek Dlhopolcek, Balozi wa Ukraine
hapa nchini Mhe. Yevheni Tsymbaliuk na Balozi wa Jamhuri ya Ghana Mhe. Kwame
Asamoah Tenkorang.
Rais Magufuli
amezungumza na Mabalozi hao kwa nyakati tofauti baada ya kupokea hati zao za
utambulisho, ambapo wamesisitiza umuhimu wa kuendeleza na kuimarisha uhusiano
na ushirikiano kati ya Tanzania na nchi hizo kwa kujikita zaidi katika biashara
na uwekezaji.
"Mhe. Balozi
najua nchi yenu ya Sudan ina utajiri wa mafuta na imefanikiwa kujenga uchumi
wake kupitia mafuta, sisi pia hapa nchini tumebaini uwepo wa mafuta na gesi
asilia katika maadhi ya maeneo, ningependa uhusiano na ushirikiano wetu sasa
ujielekeza katika kubadilishana uzoefu na ujuzi wa namna tunavyoweza kunufaika
na mafuta na gesi" amesema Rais Magufuli alipokuwa akizungumza
na Balozi wa Sudani hapa nchini Mhe. Mahjoub Ahmed Abd Allah Sharfi.
Dkt. Magufuli pia
ametoa wito kwa wafanyabiashara na wawekezaji kutoka nchi za Sudan, Slovakia,
Ukraine na Ghana kuja kuwekeza hapa nchini katika sekta mbalimbali zikiwemo
Mafuta na gesi, Kilimo, Uvuvi, Mbuga za wanyama, Madini na ufugaji.
"Hivi sasa
Tanzania ipo katika mpango wa ujenzi wa viwanda na pia tunatekeleza mpango wa
pili wa maendeleo, hivyo nakuomba Mhe. Balozi uwahamasishe wafanyabiashara na
wawekezaji wa Ukraine waje wawekeze katika viwanda kwani soko la uhakika la
bidhaa lipo" amesisitiza Dk. Magufuli
alipokuwa akizungumza na Balozi wa Ukraine hapa nchini Mhe. Yevheni Tsymbaliuk.
Aidha, Rais
Magufuli amewasihi Mabalozi wa Slovakia, Ukraine na Ghana ambao makazi yao ya
Ubalozi yapo Mjini Nairobi nchini Kenya kuanzisha Ubalozi wao hapa nchini ili
kuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano katika masuala ya biashara na
uwekezaji.
Gerson
Msigwa
Mkurugenzi
wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es
Salaam.
No comments:
Post a Comment