Kaimu Meneja Mradi wa uboreshaji wa huduma za umeme jijini Dar es Salaam, Mhandisi Iddi Rashidi, akizungumzia kukamilika kwa ujenzi wa mfumo wa njia ya kusafirisha umeme ardhini, (Underground Transmission Lines), kwenye shule ya sekondaru ya wasichana Jangwani jijini Dar es Salaam, Oktoba 22, 2016.
NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
SHIRIKA la umeme nchini (TANESCO), limekamilisha
ujenzi wa mfumo wa njia ya usafirishaji
umeme chini ya ardhi, (Underground Transmission Lines) , kutoka shule ya sekondari ya wasichana ya
Jangwani jijini Dar es Salaam na kutoka kituo cha umeme cha Makumbusho kwenda
kituo kipya cha kupozea umeme kilichoko katikati ya jiji cha City Centre cha
ukubwa wa 100MVA (2X50MVA), 132/33KV.
Akizungumzia maendeleo ya utekelezaji
wa mradi wa uboreshaji wa huduma za umeme jijini Dar es Salaam, Kaimu Meneja wa
Mradi huo, Mhandisi Iddi Rashidi, alisema, kukamilika kwa ujenzi wa mfumo huo ambao utahusisha ujenzi wa mfumo wa
njia za usambazaji umeme chini ya ardhi (Underground Distribution Lines), wa
kilomita 4.3 wa msongo wa kilovolti 33 kwa ajili ya kuunganisha kituo cha City
Centre na vituo vingine vitatu vya Kariakoo, Railway na Sokoine.
Akifafanua zaidi, Mhandisi Rashidi
alisema, ujenzi wa mfumo wa njia ya usafirishaji umeme chini ya ardhi
(Underground Transmision Lines), kwa
msongo wa Kv132 kutoka Makumbusho kwenda kituo cha City Centre tayari umekamilika
na ule wa kutoka shule ya sekondari ya wasichana Jangwani kwenye City Centre
pia umekamilika.
“Faida kubwa ambayo wakazi wa jiji la
Dar es Salaam watarajie ni kupata umeme wa uhakika (reliable power supply ulio
kwenye viwango stahiki, (Acceptable quality power supply) hususan kwa wale wa
maeneo ya katikati ya jiji,” Aliongeza Meneja wa TANESCO Mkoa wa Ilala,
Mhandisi Athanasius Nangali.
Akieleza zaidi, Mhandisi Nangai
alisema, “Mradi huu unaviwezesha viituo tajwa kuwa na njia mbili za kuvvipatia
umeme na hivyo kuwezesha kuwa na njia mbadala ya kupata umeme endapo njia moja
kati ya hizo itakuwa na hitilafu.” Alifafanua.
Alisema kuongezeka kwa kituo cha City
Centre cha 100MVA, kunafanya jiji la Dar es Salaam pekee kuwa na jumla ya vituo
9 vya aina hiyo.
“Hivi sasa tunaweza kusema, ujenzi
umekamilika kwa zaidi ya asilimia 98, kinachoendelea ni kukamilisha ujenzi wa
mfumo wa njia ya kusafirisha umeme kupitia juu (Overhead Transmission Lines), wa
kilomita 1.3 wa msongo wa kilovolti 132 kutoka kituo kikubwa cha kupozea umeme
cha Ilala hadi shule ya sekondari ya wasichana Jangwani ambapo utaungana na
mfumo wa usafirishaji umeme chini ya ardhi, (Underground Transmission Lines)
kwenda kituo kikubwa cha City Centre.” Alifafanua.
kutoka Makumbusho kwenda kituo cha
City Centre, umekamilikakatikati yan jiji utekelezaji wa Mradi huo,
unaofadhiliwa kwa pamoja na Serikali ya Tanzania na Finland, unahusisha ujenzi
wa kituo cha udhibiti mifumo ya usambazaji umeme (Distribution SCADA System),
katika msongo wa kilovolti 33 na 11.
“Tayari ujenzi wa kituo cha City
Centre umekamilika kwa asilimia 100 na sasa tuko katika hatua za majaribio.”
Alisema Mhandisi Rashidi.
Naye Kaimu Meneja Uhusiano wa
TANESCO, Bi. Leila Muhaji, amewaomba wakazi wa jiji kuwa wavumilivu wakati
zoezi hili la kuboresha miundombinu likiendelea kwani huwa panatokea kukatika
kwa umeme sehemu Fulani Fulani ili kutoa nafasi kwa mafundi kufanya kazi kwa
usalama zaidi.
No comments:
Post a Comment