HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 30, 2016

TEF YAOMBA MUDA ZAIDI KUJADILI MUSWADA WA SHERIA YA HUDUMA ZA HABARI


Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile akifafanua jambo jijini Dar es Salaam, kuhusu muswada wa Sheria ya Huduma za Habari. Wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa TEF, Theophil Makunga na Katibu wa TEF, Neville Meena. (Picha na Francis Dande) 
 Katibu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Neville Meena akifafanua jambo.
Mwenyekiti wa Jukwaa wa Wahariri, Theophili Makunga akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaa, kuhusu Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari.

Msimamo wa TEF 

Tumesikia Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, Peter Serukamba akisema kuwa Bunge litaendelea  na mchakato wa kutunga sheria hata kama sisi wadau hatukupeleka maoni.

Amekwenda mbali zaidi akatuhumu kuwa tangu mwaka 1992 tumekuwa tukikwaza sheria hii.
Tunaomba ieleweke kwamba siyo dhamira yetu  kukwaza utunzi wa sheria na wala hatupingi kutungwa kwa sheria hii.

Tuliwasilisha maombi yetu ya kuongezewa muda mbele ya Kamati ,hivyo ingetosha kwa mwenyekiti kusema maombi yamekataliwa badala ya kutoa tuhuma zisizo za msingi.

Licha ya kauli yake, bado tunaamini kuwa fursa ipo,
Tunaliomba Bunge lifikirie upya maombi yetu ,tupewe muda wa kujadiliana  na mungu akitupa uzima basi sheria  ipelekwe Bunge  la Februari kama tunavyoomba.

Ikiwa bunge na serikali wataamua kuendelea na mchakato ,hatuwezi kuwazuia maana wanatekeleza wajibu wao wa kikatiba na kisheria.

Hatuna mamlaka hayo ,ila kwa upande wetu ,tunafurahi kwamba tumetekeleza wajibu wetu wa kusema kile  tunachookiamini na Umma umetambua kwamba sisi wadau wa habari siyo sehemu ya sheria itakayowasilishwa katika Bunge linaloanza keshokutwa.

No comments:

Post a Comment

Pages