Mkuu wa Wilaya ya Chunya Rehema Madusa |
Na Mwandishi etu, Chunya
Mkuu wa Wilaya ya Chunya Rehema Madusa ameitaka halmashauri ya wilaya
ya Chunya kuhakikisha kwamba tozo zote za vijiji za Maliasili zinatozwa na zinaonekana
kwenye taarifa ya mapato na matumizi.
Aidha ameitaka halmashauri kuingiza takwimu halisi za mazao yote yanayo toka
katika maeneo ya vijiji husika.
Agizo hilo, amelitoa leo baada ya kutembelea na kukagua shughuli za kilimo cha umwagiliaji
zinazoendelea katika skimu ya Ifumbo, ambayo serikali imewekeza kiasi cha
shilingi milioni 900.
Amesema, licha ya serikali kuwekeza kiasi hicho cha fedha, bado
eneo hilo linakabiliwa na changamoto ya ukusanyaji wa mapato kwani asilimia
kubwa ya mapato hayo yamekuwa hayakusanywi
ipasavyo kutokana na kukithiri kwa njia za panya.
“Serikali inapoteza fedha nyingi na hii inatokana na kutokuwepo
kwa mfumo bora wa ufutiliaji wa mazao
hivyo mchakato huo utasaidia kuongeza mapato katika Wilaya na halmashauri
yenyewe,”amesema.
Hata hivyo, amesema nguvu kubwa iliyopo sasa ni kudhibiti njia
zote za panya hasa katika eneo la Shoga ambalo ndio eneo linalotumiwa zaidi na
wafanyabiashara wasio waaminifu.
No comments:
Post a Comment