HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 12, 2016

GOLF IJUMUISHWE MICHEZO YA MAJESHI AFRIKA MASHARIKI -WAITARA

 Aliyekuwa Mkuu wa Majeshi Jenerali mstaafu George Waitara akizungumza na baadhi ya wanafunzi waliojitokeza kupata mafunzo ya mchezo wa golf katika Klabu ya Jeshi la Wananchi Tanzania ya Lugalo jijini Dar es Salaam. (Picha na Luteni Selemani Semunyu)
Aliyekuwa Mkuu wa Majeshi Jenerali mstaafu George Waitara akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Kombe la Waitara.

Na Luteni  Selemani Semunyu JWTZ

Aliyekuwa Mkuu wa Majeshi  ya Ulinzi Jenerali Mstaafu George Waitara amesema wakati umefika sasa kwa Michezo ya  Majeshi kwa nchi za Afrika Mashariki kujumuisha mchezo wa Golf kutokana na idadi kubwa ya maofisa na Askari wanaojitokeza kucheza mchezo huo katika Nchi hizo.

Aliyasema hayo Leo  Jijini Dar es salaam wakati akizungumza na Waandishi wa habari kufuatia kuanza kwa Maandalizi ya Kombe la Waitara linalotarajiwa kufanyika Novemba 19 Mwaka huu katika Viwanja vya Jeshi vya Lugalo.

“Ukiangalia Uongozi mpya na mkakati iliofanya na idadi kubwa ya Maofisa na Askari walioanza kujitokeza kujifunza mchezo huo  ni ishara tosha kuwa wakati umefika kwa mchezo huo kuingizwa katika michezo itakayoshindaniwa katika Michezo ya majeshi kwa kuwa na nchi nyingine pia wapo,Alisema Jenerali Waitara.

Aliongeza kuwa  ni furaha yake ikiwa ni miaka kumi tangu kuanzishwa na mwitikio kuwa mkubwa hivyo anaimani miaka ijayo kutakuwa na idadi kubwa zaidi na hivyo kuomba waaandishi wa habari kuendelea kuutangaza mchezo huo.

Akizungumzia Maandalizi ya Mashindano ya Kombe lake aliahidi kikundi chake kinachocheza ndani ya Klabu ya Lugalo na “Generals Four Balls” kitafanya vizuri katika mashindano hayo licha ya umri mkubwa walionao.

Aliwataja washiriki wa Kikundi hicho kuwa ni Yeye Binafsi Jenerali Mstaafu  Waitara, Balozi Charles Sanga , Dk Edmund Mndolwa na Katibu Mkuu wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mh Job Masima na kuwataka wengine pia kuanzisha vikundi vya Ushindani ndani ya Klabu ili kuongeza hamasa.

 Jenerali Waitara aliwataka wachezaji wengi kujitokeza kushiriki katika  mashindano hayo kutokana na historia yake lakini kupunguza gharama kwa wachezaji kwa kuwa uwanja pekee wa kizalendo nchini huku gharama zikiwa chini  ukilinganisha na viwanja vingine.

 Kwa Upande Wake Balozi Charles Sanga alishukuru  JWTZ kwa kuamua kuanzisha uwanja lakini pia kwa mwanzilishi wa Uwanja kutokana na Ukweli kuwa Uwanja Wa Golf wa Lugalo  umekuwa kimbilio kwa Watu wote kutokana na uzuri wake na gharama kuwa za chini.

No comments:

Post a Comment

Pages