Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu (kushoto), akimsiliza Meneja wa TEMESA Njombe Mhandisi John Rubaga (kulia) wakati alipotembelea kituoni hapo kujionea utendaji wa kazi wa kituo hicho.
Watumishi wa TEMESA Njombe wakimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu (Mwenye shati la rangi ya bluu) alipotembelea kituoni hapo kujionea utendaji wa kazi wa kituo hicho. Picha zote na Theresia Mwami TEMESA Njombe.
Na Theresia Mwami TEMESA Njombe
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu ameahidi kuwapatia makasha yenye vitendea kazi vya karakana pamoja na mashine ya kucharge betri za magari kwa wafanyakazi wa kituo cha TEMESA Mkoani Njombe.
Dk Mgwatu amesema kuwa ameamua kuleta mabadiliko katika ufanyaji kazi kwa kuhakikisha wafanyakazi wanapata vitendea kazi kwa ajili ya kutekeleza majukumu yao ya kila siku.
“Nitaleta vifaa vinavyohitajika nataka kila mmoja atimize wajibu wake, tufanye kazi kwa kuzingatia uadilifu sababu tunabeba dhamana kubwa ya kutengeneza magari ya viongozi mbali mbali wa serikali” alisema Dkt Mgwatu.
,Mtendani huyo ameongeza kuwa atokuwa na msamaha na mtumishi yeyote atakayeshindwa kuwa muadilifu na kutoimiza wajibu wake ipasavyo.
Aidha Dkt Mgwatu aliwaagiza watumishi wa kituo hicho kufanya kazi kwa weledi na kwa ubora zaidi ili karakana iweze kuvuta wateja wengi zaidi na kuongeza pato la kituo.
Kwa upande wake Kaimu Meneja wa TEMESA Njombe Mhandisi John Rubaga alimueleza kuwa kituo kinakabiliwa na tatizo la madeni kinayodai wateja wake pamoja na madeni kinayodaiwa na wazabuni mbali mbali.
Mtendaji Mkuu wa TEMESA Dkt. Musaa Mgwatu yupo katika ziara ya kikazi kutembelea vituo vya TEMESA vilivyopo nyanda za juu Kusini ili kubaini changamoto mbali mbali zilizo kwenye vituo hivyo na kuzitafutia ufumbuzi.
No comments:
Post a Comment