Mami ya wananchi wamehudhuria maziko ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Dimani Hafidhi Ali Tahir yaliofanyika maungani jana.
Mwili wake uliwasili jana majira ya saa 7 mchana ukitokea mjini Dodoma ambapo katika uwanja wa ndege wa Zanzibar ulipokelewa na viongozi mbalimbali wa vyama na serikali pamoja na familia yake.
Mwili wa marehemu huyo baada ya kupokelewa, ulipelekwa hadi nyumbani kwao Maungani kwa taratibu za mazishi.
Ambao saa kumi kamili mwili huo ulipelekwa katika maeneo ya makabu masafa madogo kutoka nyumbani kwake huko katika kijiji cha maungani.
Akizungumza juu ya msiba huo, Katibu wa Chama cha Mapinduizi Wilaya ya Dimani, Yahya Saleh Issa, alisema Wilaya yake wamekipokea kifo hicho kwa mshituko mkubwa kwani marehemu alikuwa mtu wa watu na katika nafasi yake alikuwa anaitekeleza ilani ya chama kwa mafanikio.
Hivyo aliwataka wananchi wa jimbo hilo kuwa wastahamilivu na kuendelea kumuombea marehemu.
Kwa upande wa chama cha mapinduzi, kwa upande wa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai alisema Chama cha Mapinduzi kinaungana na wanafamilia katika wakati huu mgumu na kwamba wamekipokea kifo hicho kwa mshituko mkubwa, lakini kazi ya Mungu haina makosa.
Viongozi walihudhuria mazishi hayo ni Pamoja Waziri wa Ulinzi Hussein Mwinyi, Naibu Wazri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni na Mbunge wa Sengerema, Wiliam Ngeleja na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge, Mussa Azan Zungu.
Mtoto wa marehemu Is-haka Hafidh Ali, alisema kuwa kifo cha baba yao wamekipokea kwa mshituko kwani kilikuwa cha ghafla na ameiomba Serikali kuwa karibu nao pamoja na kuwajali kwani baba yao aliwahi kuitumikia serikali na chama cha ujumla.
Alisema marehemu baba yao alikuwa mtu wa watu na kuwa karibu na watu wengi hivyo wamepata pengo kubwa kwa kuondokewa .
Marehemu Hafidh alizaliwa Oktoba 30 mwaka 1953 na kufariki dunia akiwa na umri wa miaka 63 na ameacha kizuka mmoja na watoto saba.
No comments:
Post a Comment