Mlezi wa Kamati ya Miss Tanzania ambaye pia Balozi wa Heshima wa Botswana nchini Tanzania, Bw. Emanuel Ole Naiko akimkabidhi bendera Diana Edward Lukumai Miss Tanzania 2016 anayeondoka nchini kesho kuelekea nchini Marekani kwa ajili ya Shindano la Miss Word linalotarajiwa kufanyika nchini humo, Katikati ni Hashim Lundenga Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania, Hafla hiyo imefanyika leo kwenye hoteli ya New Africa jijini Dar es salaam.
Diana Edward Lukumai Miss Tanzania 2016 akizungumza mbele ya waandishi wa habari leo kwenye hoteli ya New Africa Jijini Dar es salaam wakati alipokabidhiwa bendera ya Taifa kwa ajili ya safari yake ya Marekani atakakoshiriki shindano la dunia la Miss Word, Kulia ni Mkuu wa Itifaki Miss Tanzania Bw. Albert Makoye na katikati ni Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania Bw. Hashim Lundenga.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Mapema mwezi Machi 2016 tulishuhudia uzinduzi wa mashindano ya Miss Tanzania, uzinduzi ambao ulifanyika katika Hotel ya Ramada iliyopo eneo la ufukwe wa bahari ya Hindi Kunduchi.
Uzinduzi wa mashindano ya urembo ya Miss Tanzania 2016 mwezi Machi kulianzisha marathoni ya kumtafuta Miss Tanzania 2016 mashindano ambayo yalifanyika katika mikoa mbalimbali nchini na hatimae kuweza kumpata mrembo wa Taifa, Miss Tanzania 2016 Diana Edward Lukumai ambaye leo hii tunamuaga aweze kutuwakilisha vema katika Mashindano ya urembo ya Dunia ambayo kwa mwaka huu yatafanyika Washington DC nchini Marekani.
Katika miaka 22 ya Mashindano ya urembo ya Miss Tanzania, miaka yote hiyo Fainali za shindano la Miss Tanzania lilikuwa likifanyika jijini Dar es salaam, lakini kwa mwaka huu 2016 kwa mara ya kwanza Fainali hizi zimefanyika jijini Mwanza, na napenda kuchukua fursa hii kuwashukuru wakazi wa Mwanza na vitongoji vyake kuweza kujitokeza kwa wingi katika Fainali zile ambazo zilifanyika katika ukumbi wa Rocky City Jijini Mwanza.
Mshindi ameshapatikana ni mrembo wetu kutoka Kanda ya Kinondoni, Kituo cha Ubungo. Miss Tanzania 2016 Diana Edward Lukumai na leo hii tupo hapa kumfanyia sherehe maalumu ya kumuaga na kumtakia kila la heri katika safari yake hii kuelekea Mashindano ya urembo ya Dunia tukiwa na matumaini makubwa kwamba utatuwakilisha vema na kujerea na Taji la Mrembo wa Dunia, yaani Miss World 2016.
No comments:
Post a Comment