Na Abel Daud
Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Col. Martin Mkisi ametoa siku saba kwa wananchi wate wanaofanya shughuli za kilimo na ufugaji wa mifugo pamoja na uchomaji wa mkaa ndani ya msitu wa hifadhi ya taifa makele kaskazini na makele kusini kuondoka mara moja kabla ya hatua kali za kisheria hazijachukuliwa.
Hayo ameyasema alipofanya ziara ya kutembelea baadhi ya maeneo ndani ya hifadhi hiyo yaliyo haribiwa na wananchi kwa shughuli za kilimo na ufugaji vinavyofanywa kinyume cha sheria.
Col.Mkisi ameeleza kuwa Serikali ya Wilaya kupitia kamati ya ulinzi na usalama tayari wamepitisha mapendekezo ya kuanza kutolewa elimu kwa wananchi juu ya utunzaji wa hifadhi hyo kupitia kwa viongozi wa vijiji pamoja na watendaji wa vijiji, pia amewatahadharisha wananchi wa Tanzania Wilayani hapo wanaojihusisha na tqbia ya kuwapokea na kuwahifadhi wahamiaji haramu kuacha mara moja na kuwaeleza hatua kali zitachukuliwa kwa yeyote atakaye bainika.
Naye Kaimu afisa uhamiaji wa Wilaya ya kasulu Bw.Emmanuel Mpayo amekiri kuwepo kwa wimbi la wahamiaji haramu ndani ya msitu wa hifadhi ya taifa wa makele wanaojihusisha na shuguli za kilimo na ukataji wa mkaa,ameongeza kuwa tatizo hilo linatokana na Watanzania wasiokuwa wazalendo kwa nchi yao kwa kukubali kuwapoke kwa ajili ya wakuwatumikisha katika shughuli za kilimo na kuutaka uongozi wa Wilaya kupitia vyombo vya ulinzi na usalama kushirikiana kudhibiti mipaka na njia wanazopitia wahamiaji hao kuingia nchini.
Kwa upande wake Kaimu Maneja wa wakala wa misitu Tanzania(TFS) wilayani kasulu ndg.William Sikoi ameeleza kuwa kuanzia mwaka 2013-2016 wamefanikiwa kukamata ng'ombe 8498,na baada ya faini kulipwa Serikali imefanikiwa kupata tsh.199 million,pamoja na mafanikio hayo pia ameeleza changamoto zinazowakabili kuwa ni pamoja na upungufu wa vitendea kazi na swala zima la siasa, na kuwataka wanasiasa kuacha kuwashawishi wananchi kuingia na kufanya shughuli za kilimo na ufugaji ndani ya hifadhi hyo na kwamba kwa sasa uchaguzi umekwisha zaidi wajikite katika kufanya kazi.
No comments:
Post a Comment