HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 08, 2016

MWILI WA SPIKA MSTAAFU SAMUEL SITA KUWASILI NOVEMBA 10

Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Emmanuel Nchimi akimfariji mtoto wa Spika mstaafu, Benjamin Sitta nyumbani kwao Msasani Peninsula jijini Dar es Salaam, mwili wa marehemu Samuel Sitta utawasili Novemba 10 ukitokea katika nchni Ujerumani alikokuwa amekwenda kupata matibabu ya saratani ya tezi dume. Novemba 11 mwili wake utaagwa katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam na baadae kusafirishwa hadi mkoani Dodoma kwa ajili ya kutoa fursa kwa Wabunge kutoa heshima zao za mwisho.  (Picha na Francis Dande)
 Mbunge wa zamani wa Kahama, James Limbeli akimpa pole Benjamin Sitta.
Mbunge wa zamani wa Mafia, Abdulkarim Shah akisaini kitabu.
 Lembeli akisaini kitabu cha maombolezo.
 Waziri wa zamani, Prof. Philemon Sarungi akimpa pole Agnes Sitta ambaye ni mtoto wa Spika mstaafu, marehemu Samuel Sitta nyumbani kwao Msasani Peninsula jijini Dar es Salaam
 Pole sana.
Aliyekuwa mbunge wa Mafia, Abdulkarim Shah (katikati) na mbunge wa zamani wa Kahama, James Lembeli (kulia), wakimfariji mtoto wa Spika mstaafu marehemu Samuel Sitta nyumbani kwao Msasani Peninsula jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Pages