Mkurugenzi wa Huduma za Sheria, Bw. Onorius Njole akitoa mada ya masuala ya baadhi ya Miongozo iliyotolewa na Mamlaka ili kuboresha utendaji katika Sekta ya Hifadhi ya Jamii kwa Mameneja na Maafisa wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, Mkoani Morogoro hivi karibuni.
Mkurugenzi wa Tafiti, Tathmini na Sera, Bw. Ansgar Mushi
akifafanua jambo la kitaalamu katika Semina iliyotolewa na SSRA
kwa Mameneja na Maafisa wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, mkoani Morogoro hivi karibuni.
Mameneja na Maafisa wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wakisikiliza kwa makini mada zilizokuwa zikitolewa na watoa mada toka
SSRA katika Semina ya kuwajengea uwezo wa kiutendaji katika Sekta ya Hifadhi ya Jamii.
Meneja wa Huduma za Kisheria akitoa maelezo ya mmoja ya mada zilizokuwa zikiendelea katika Semina toka
SSRA kwa Mameneja na Maafisa wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.
Mwanasheria Mwandamizi, Bw. Omar
Sururu akieleza na kufafanua jambo la kisheria katika Miongozo iliyotolewa na SSRA,
Katika Semina iliyofanyika kwa lengo la
kuwajengea uwezo Mameneja na Maafisa wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.
Mmoja ya washiriki wa Semina kutoka Mifuko ya Hifadhi ya Jamii akiuliza swali na kuhitaji ufafanuzi baada ya mada zilizotolewa na Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii.
Picha ya Pamoja ya Wafanyakazi wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii wakiwa na Mameneja na Maafisa wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii baada ya Semina iliyofanyika kwa lengo la kuwajengea uwezo na kuongeza ufanisi katika Sekta ya Hifadhi ya Jamii, iliyofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoani Morogoro hivi karibuni.
No comments:
Post a Comment