Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu, Bunge, Kazi,
Ajira na wenye ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama, akikata utepe kuzindua mafao ya Fidia na na ubia baina ya watoa huduma za afya .Uzinduzi huo ulifanywa na Waziri Mhagama kwa
niaba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa jijini Dar es Salaam, Desemba 20, 2016. wanaoshuhudia ni Naibu Mawaziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Mh. Anthony Mavunde, (wapili kulia), Mh. Dkt. Abdallah Possi, (watatu kulia), Bw. Emmanuel Humba, Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), wanne kulia, na Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba. (watano kulia).
.(
PICHA NA MUHIDIN SUFIANI)
NA ANTHONY JOHN, GLOBU YA JAMII
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera,Bunge kazi ,vijana Ajira
na watu wenye ulemavu, Jenista Muhagama, amewataka waajili wote kuwasilisha
Michango ya wafanyakazi wao Mfuko Fidia kwa Wafanyakazi WCF kwa wakati.
Akizungumza katika Uzinduzi wa Huduma za utoaji wa Mafao ya fidia
kwa wafanyakazi na ubia kati ya Mfuko na watoa Huduma za Afya amesema kuwa
kwa Mwaka huu wafedha Serikali imewasilisha Michango ya
wafanyakazi wake wote ambapo alizitaka Sekta binafsi pia kuwasilisha Michango
yao kwa wakati.
Sanjari na Hayo Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo Masha Mshomba
ameongeza kuwa Mpaka kufikia Novemba 30 Mwaka huu Jumla ya waajili 5945
wamechangia na wamepewa na ya usajili.
Hata Hivyo Mweketi wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mfuko huo
Emmanuel Humba amesema Mfuko Huo utachangia kwa kiwango kikubwa Sera ya
Tanzania ya Viwanda iliyoa anzishwa na Serikali ya awamu ya tano kwani
wafanyakazi watakapo kuwa na Afya njema watafanya kazi kwakujiamini na
kuleta Maendeleo.
Waziri Mhagama akihutubia
Mwenyekiti wa bodi ya WCF, Bw. Emmanuel Humba akitoa hotuba yake
Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw.Masha Mshomba, akitoa hotuba yake
Mgeni rasmi, Naibu Mawaziri, viongozi wa WCF, na waliotunukiwa vyeti wakiwa kwenye picha ya pamoja
<!--[if gte mso 9]>
No comments:
Post a Comment