HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 11, 2016

RAIS WA FIFA ATUMA SALAMA ZA RAMBIRAMBI KIFO CHA MCHEZAJI WA MBAO FC

Rais wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu Ulimwenguni (FIFA), Bw. Gianni Infantino ametuma salamu za rambirambi kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Bw. Jamal Emil Malinzi kutokana na kifo cha ghafla cha Mchezaji.
Mchezaji aliyekutwa na mauti ni Ismail Mrisho Khalfan. Alifariki dunia baada ya kuanguka uwanjani Desemba 4, 2016 kwenye Uwanja wa Kaitaba, Kagera wakati timu yake ya Mbao ikicheza na Mwadui katika mechi ya ligi ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 20.
Rais Infantino, katika salamu zake kwa Rais Malinzi, alianza kwa kusema: “Tafadhali pokea salamu zangu za rambirambi baada ya kusikia kifo cha Mchezaji Ismail Mrisho Khalfan ambaye ni mchezaji mwenye umri wa chini ya miaka 20.
“Kwa niaba ya Wajumbe wa kimataifa wa mpira wa miguu, sina budi kutuma salamu hii hizi kwa familia nzima ya mipira wa miguu duniani na familia ya Khalfan iliyopoteza mpendwa wao.”
Mchezaji Ismail Mrisho Khalfan wa timu ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 20 wa Mbao FC ya Mwanza, kilitokea Desemba 4, 2016 kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba mkoani Kagera wakati timu yake ikicheza mchezo huo dhidi ya Mwadui FC ya Shinyanga.
Salaam Rais Infantino, zinakwenda sambamba na za Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wa Tanzania, Ndugu Nape Nnauye na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Issa Hayatou.
Timu hiyo ya Vijana wa Mbao, kama vilivyo timu nyingine 7 za Ligi kuu ya Vodacom, ilikuwa Kituo cha Bukoba katika Ligi ya avijana ambayo kwa msimu huu imefanyika kwa mara ya kwanza. Timu nyingine Nane zilikuwa kituo cha Dar es Salaam.
Ismail aliyeanguka uwanjani dakika ya 74, alipata huduma ya kwanza uwanjani hapo kwa madaktari waliokuwa uwanjani, lakini baadaye taarifa za kitabibu zilionyesha amefariki dunia.
Kamati ya Tiba ya TFF, bado inaendelea na uchunguzi wa kifo cha mchezaji huyo kabla ya baadaye kutoa taarifa za kamili ya kitatibu kujua hasa chanzo hasa cha kifo cha mchezaji huyo ambaye mwili wake umehifadhiwa kwenye Hospitali ya Mkoa Kagera. Marehemu Ismail Mrisho Khalfan alizikwa Desemba 5, 2016 jijini Mwanza. 

No comments:

Post a Comment

Pages