HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 19, 2017

SERIKALI IMETENGA FEDHA KUKAMILISHA UJENZI TERMINAL III

 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, Salim Msangi akimkaribisha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa alipofanya ziara leo Januari 19 kuangalia Ujenzi wa Jengo la Tatu la Abiria (TB III), katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere. (Picha na Francis Dande).
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, Salim Msangi akitoa maelezo ya Utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa Jengo la Tatu la Abiria (TB III), katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa. 
Kukagua Mradi wa Ujenzi.
 Waziri Mbarawa (katikati), akisikiliza kwa makini maelezo ya Mhandisi Mohamed Millanga kuhusu ujenzi huo.
 Mkurugenzi wa Mradi Mhandisi Mohamed Millanga akitoa maelezo kwa Waziri Mbarawa.
 Waziri Mbarawa akikagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa jengo la tatu la abiria (TB III) katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere.  
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliamo, Prof. Makame Mbarawa (kushoto), akipata maelezo kuhusu ujenzi wa jengo la tatu la abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), kutoka kwa Mkurugenzi wa Mradi Mhandisi Mohamed Millanga wakati waziri alipofanya ziara jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, Salim Msangi.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliamo, Prof. Makame Mbarawa akizungumza mara baada ya kukagua ujenzi wa ujenzi wa jengo la tatu la abiria (TB III) katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere.  Kulia ni Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, Salim Msangi.

xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx


Serikali imesema itatoa fedha kwa ajili ya kukamilisha sehemu ya pili ya mradi wa ujenzi wa  Jengo la Abiria la Tatu la abiria (Terminal III) katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam ili kuboresha huduma za  usafiri wa anga nchini.

Akizungumza mara baada ya kukagua mradi huo Waziri Prof. Makame Mbarawa amesema ujenzi wa mradi huo sehemu ya kwanza ilifadhiliwa na Benki ya HSBC ya Uingereza hivyo sehemu ya pili Serikali itatoa fedha  ili kukamilisha mradi huo.

”Awamu ya kwanza ya ujenzi huu tulipata mkopo lakini awamu ya pili ya mradi Serikali tumesema hatutachukua mkopo, tutajenga kwa fedha zetu za ndani sababu tuna uzoefu mkubwa wa utekezaji wa miradi kwa kutumia fedha za zetu za ndani'' amesema Prof. Mbarawa.

Aidha, Prof. Mbarawa ameongeza kuwa imarishaji wa viwanja vya ndege nchini unakwenda  sabamba na uimarishaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) ambao mpaka sasa tayari lina ndege mbili aina ya Bombadier Q400.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Salim Msangi , amesema mpaka mwishoni mwa mwanzoni wa Mwaka huu mradi huo umekamilika kwa asilimia 66 na kazi zinazoendelea kwa sasa ni kuezeka na kumalizia kazi za ndani ya jengo ikiwemo usimikaji wa mitambo ya umeme, viyoyozi na utandikaji wa nyaya na mbomba kwa ajili ya miundombinu ya ndani.

Ameongeza kuwa kazi za nje ya jengo zinazohusisha  maegesho ya ndege yamekamilika kwa asilimia 53, maegesho ya magari asilimia 36  na  eneo la mitambo na umeme asilimia 46.
Bw. Msangi amesema kuwa mpaka kufikia mwaka 2020 idadi ya abiria wanaotumia kiwanja cha JNIA watafikia milioni 5 kwa mwaka na makadirio ifikapo mwaka 2025 idadi itaongezeka watafiia milioni 5 kwa mwakaa.

Mradi huu wa jengo la mita za mradi za mraba sitini elfu unatarajiwa kukamilikak mwezi Desemba Mwaka huu na utahudumia abiria zaidi ya milioni 6 kwa mwaka na litaweza kuhuduumia abiria 2,700 kwa saa na litakuwa na uwezo wakuhudumia ndege kubwa aina ya Airbus A380.

No comments:

Post a Comment

Pages