SHIRIKA LA TAIFA LA
HIFADHI YA JAMII (NSSF) LINAPENDA KUUTAARIFU UMMA KUWA LEO SIKU YA JUMATATU TAREHE 13/02/2017 MAJIRA YA SAA NANE
MCHANA KULIZUKA MOTO KATIKA JENGO
LA NSSF WATER FRONT DAR ES SALAAM, NA
KUZUA TAHARUKI KWA WATU WENGI NDANI NA NJE YA JENGO HILO.
TAARIFA ZA AWALI
ZINAONYESHA KUWA MOTO HUO ULITOKANA NA KUUNGUA KWA BAJAJI ILIYOKUWA IMEEGESHWA
KATIKA MAEGESHO YA CHINI YA JENGO. HATA HIVYO TAARIFA KAMILI ZITATOLEWA BAADA
YA UCHUNGUZI KUPITIA VYOMBO HUSIKA KUKAMILIKA.
MOTO HUO ULIZIMWA
KWA USHIRIKIANO WA VIKOSI VYA ZIMAMOTO NA WANANCHI NA HAKUNA MADHARA YA
KIBINADAMU AU MALI YALIYOTHIBITIKA KUTOKEA HADI SASA MBALI NA KUTEKETEA KWA
BAJAJI HIYO.
SHIRIKA LINATOA
SHUKRANI KWA VYOMBO VYOTE PAMOJA NA WANANCHI WALIOTOA USHIRIKIANO KUDHIBITI
MOTO HUO.
IMETOLEWA NA IDARA YA MASOKO NA UHUSIANO, NSSF MAKAO MAKUU
No comments:
Post a Comment