SAFARI ya kuelekea Tamasha la Muziki wa injili la Pasaka litakalofanyika April 17, jijini Dar es Salaam kabla ya kugeukia mikoani, imeanza.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Msama Promotions Ltd ya jijini Dar es Salaam inayoratibu tamasha
hilo, Alex Msama alisema, kwa sasa wanazidi kujipanga.
“Tunashukuru
Mungu, japokuwa tunasubiri kibali cha Basata (Baraza la Sanaa Tanzania),
maandalizi ya awali tayari tumeanza,” alisema Msama.
Alisema
baada ya kuzinduliwa jijini Dar es Salaam April 16, kivumbi cha shangwe za
tamasha hilo kitahamia katika mikoa itakayokuwa imepitishwa na kamati.
“Ingawa
Kamati haijaanza rasmi kupokea maombi ya mikoa ambayo ingetaka kufikiwa na
tamasha la Pasaka, tayari mikoa kadhaa hadi sasa imeonyesha kulitaka,” alisema.
Msama amedokeza
baadhi ya mikoa ambayo imelitaka Tamasha hilo ni Singida, Ruvuma, Iringa,
Arusha, Tanga, Shinyanga na Mwanza.
Kuhusu
waimbaji, Msama alisema mazungumzo ya awali yameanza na waimbaji wa hapa nchini
pamoja na kutoka nje kama Afrika Kusini, Kenya, Rwanda, Uingereza na Nigeria.
Msama
alisema pamoja na lengo kuu la tamasha hilo ambalo ni kueneza neno la Mungu,
tamasha la mwaka huu litatumika pia kuliombea
taifa na watu wake.
Alisema
katika mazingira yalivyo nchini, kuna haja kwa watu wa Mungu kumwombea Rais
John Magufuli azidi kumuongoza katika dhamira yake ya kupambana na maovu.
Tangu
kuanziashwa kwa Tamasha la Pasaka mwaka 2000, mbali ya kutumika kuutangaza
utukufu wa Mungu, pia likuwa faraja kwa makundi maalumu katika jamii.
Hii ni
kutokana na sehemu ya fedha ambazo zimekuwa zikipatikana kupitia viingilio,
kutumika kuwafariji walemavu, yatima na wajane kabla ama baada ya kufanyika.
No comments:
Post a Comment