Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akizungumza na waandishi wa habari (hawapo Pichani) leo Februari 07, 2017 Jijini Dar es Salaam kuhusu mkakati wa Wizara kuanza kuzungumza na wadau katika sekta zinazosimamiwa na Wizara yake. (Picha na Raymond Mushumbusi)
Na: Genofeva Matemu
Wizara
ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imebuni na kutanganza Programu ya
kushirikisha wadau inayoitwa wadau tuzungumze itakayosaidia wizara kupata
vionjo, maoni, mawazo na fikra za wadau katika kuhakikisha kwamba Wizara inafanya
kama wadau wake wanavyotegemea.
Hayo
yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof.
Elisante Ole Gabriel alipokua akizungumza na waandishi wa habari kutangaza
programu hiyo yenye kauli mbiu ya kuitoa wizara ofisini kuipeleka kwa wadau leo
Jijini Dar es Salaam.
Prof.
Gabriel amesema kuwa Wizara imekua na kauli mbiu ya kuitoa Wizara Dar es Salaam
kuipeleka mikoani na sasa inaendelea na mkakati wa kuitoa wizara ofisini na
kuipeleka kwa wadau kwani Shabaa kubwa ya wizara ni kuhakikisha kwamba yale
yanayofanywa na wizara jamii iyafahamu katika kutekeleza nia na hari ya hapa
kazi tuu ya serikali ya awamu ya tano.
“Mpango
wa programu ya wadau tuzungumze utafanyika kisekta ambapo utakua ni mkutano
utakaoshirikisha mmoja wa viongozi wa wizara kukutanana na wadau na utakua na utaratibu
madhubuti kwa kila mwezi siku ya jumanne saa nne asubuhi ambapo viongozi hao
watakutana na vyombo vya habari wakiwa na wadau kujadili mambo ya kisekta”
amesema Prof. Gabriel.
Mpango
huu utahusisha Jumanne ya kwanza ya mwezi sekta ya habari na wadau wote wa
habari, jumanne ya pili ya mwezi ni kwa ajili ya sekta ya Utamaduni na wadau
wote wa utamaduni, jumanne ya tatu ya mwezi ni kwa ajili ya sekta ya sanaa na
wadau wote wa sanaa na mwisho jumanne ya nne ya mwezi ni kwa ajili ya sekta ya
maendeleo ya michezo na wadau wake.
Pamoja
na mambo mengine program hii itatoa fursa kubwa sana kwa wadau kuleta mawazo
yao ili wizara iweze kuwaingiza kwenye mnyororo wa thamani wa shughuli zake
kwani wizara inatamani ifanye kwa mlengo ambao wadau weke wanatamani ifanyike.
Progamu
hii itazinduliwa rasmi tarehe 14 Mwezi Februari mwaka 2017 hapa Jijini Dar es Salaam ambapo itahushisha sekta ya
Utamaduni na hapo baadaye mikutano hii inaweza kufikiriwa na kufanywa kwa
kanda. Mpango huu utahusisha pia Taasisi zilizo chini ya wizara.
|
No comments:
Post a Comment