Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amewataka wasimamizi wa miradi ya
matengenezo ya barabara kuzingatia taaluma na weledi husika ili kupata
thamani ya fedha kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu husika bila
kukiuka taratibu za manunuzi.
RC
Makonda ameyasema hayo alipokuwa anafungua kikao cha bodi ya barabara
ya mkoa wa Dar es Salaam kilichofanyika katika ukumbi wa Arnautoglo na
kuwaomba mameya, madiwani, wakuu wa wilaya na wakurugenzi kuifuatilia
miradi hii kwa karibu, huku akishauri kuwa ni vyema miradi hii
ikafanyika kwa gharama nafuu, kwa muda mfupi na kwa viwango, kwani fedha
za wananchi ndiyo zinatumika wanapaswa kutendewa haki kwa kuona matokeo
chanya kwenye miradi ya maendeleo.
Huku akisisitiza kuwa katika maslahi ya wananchi hatoangalia anagombana na wangapi, atahakikisha anatimiza wajibu wake.
Katika
hatua nyingine kampuni ya ujenzi ya IBRA Contractors Limited kupitia
Mkurugenzi wake Maida Waziri ameeleza kuhusu ujenzi wa barabara
zinazotumia teknolojia ya kisasa kwa udongo wa kawaida ni bora na huweza
kudumu zaidi ya miaka 10, haina vumbi wala uterezi na ujenzi wake
hutumia muda mfupi na kuishauri serikali kutumia ujenzi huo wa gharama
nafuu kwa takribani asilimia 50, huku akizitolea mfano Australia na
Algeria kuanza kutumia ujenzi huo, hivyo hiyo ni suluhu ya lawama za
muda mrefu kuhusu barabara mbovu nchini.
Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa ujenzi huo wa kibunifu utakuwa njia ya kuvifanya vijiji kuwa miji kupitia barabara.
No comments:
Post a Comment