Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harrison George Mwakyembe na aliyekuwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye wakitia saini hati za makabidhiano rasmi ya Ofisi yaliyofanyika katika Ofisi za Wizara Mjini Dodoma akishubudia utiaji wa saini ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof Elisante Ole Gabriel.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harrison George Mwakyembe na aliyekuwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye wakikabidhiana hati za makabidhiano rasmi ya Ofisi yaliyofanyika katika Ofisi za Wizara Mjini Dodoma.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA
HABARI
Aliyekuwa
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye leo amekabidhi
rasmi ofisi kwa Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe aliyeteuliwa hivi karibuni kuwa Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Katika
makabidhiano hayo yaliyohudhuriwa na watendaji wakuu wa Wizara, Mhe. Mwakyembe
ameahidi kuwa licha ya kukabidhiwa ofisi, anaamini kuwa Mhe. Nnauye bado ni
mdau mkubwa wa sekta za Wizara na kuwa
anategemea kuendelea kupata ushirikiano kutoka kwake.
Aidha
Waziri Mwakyembe ameahidi kuendeleza yote mazuri yaliyo anzishwa na Mhe. Nnauye
katika kuimarisha ufanisi wa Wizara na kuhakikisha inakuwa ni moja ya Wizara za
mifano nchini. Amesisitiza kuwa katika kipindi kifupi alichokaa Wizarani, Mhe. Nnauye
alianzisha mabadiliko makubwa na watu wameanza kuifahamu vizuri Wizara.
Kwa upande
wake Mhe. Nnauye amemshukuru Rais John Pombe Magufuli kwa kumuamini na kumpa
dhamana kubwa ya kusimamia Wizara kwa kipindi cha miezi 15 huku akiwa ndio
kwanza amekuwa mbunge katika awamu yake ya kwanza.Aidha Mhe. Nnauye ameahidi kuendela
kushirikiana na Wizara kwa ukaribu kwani ni kweli yeye ni mdau mkubwa wa sekta
za wizara hii.
“Heshima aliyonipa Mhe. Rais ni
kubwa mno na nitaendelea kumuunga mkono katika dhamira yake njema ya kuleta
mageuzi nchini,” alisema
Mhe. Nnauye. Aidha alisisitiza kuwa, tofauti na maneno ya mitandaoni, yeye
atabaki kuwa mtiifu kwa Rais, Serikali na chama chake.
Pia amewashukuru
watendaji wote wa Wizara kwa kumpa ushirikiano wa kutosha kwa kipindi chote
alichofanya nao kazi na kuwaomba kutoa ushirikiano huo huo kwa Waziri wa sasa
Mhe. Mwakyembe.
Imetolewa na
Zawadi Msalla
Kaimu
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Wizara ya
Habari Utamaduni Sanaa na Michezo.
28/03/2017
No comments:
Post a Comment