HABARI MSETO (HEADER)

Breaking

March 02, 2017

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA KUWA MGENI RASMI MKUTANO WA TISA WA WADAU WA LAPF

 Meneja Masoko na Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, James Mlowe (wa pili kulia), akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini kuhusu mkutano na wa tisa wa wadau wa LAPF utakaofanyika jijini Arusha Machi  9-10. (Picha na Francis Dande).
 Mkutano ukiendelea.
Waandishi wa habari wakimsikiliza Meneja Masoko na Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, James Mlowe.

 Meneja Masoko na Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, James Mlowe akifafanua jambo kuhusu mkutano wa wadau wa mfuko huo. Kulia ni Meneja Takwimu, Hadhari na Tathmini, Abubakar Ndwata.

Meneja Masoko na Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, James Mlowe akifafanua jambo kuhusu mkutano wa wadau wa mfuko huo. Kulia ni Meneja Takwimu, Hadhari na Tathmini, Abubakar Ndwata. 
Meneja Masoko na Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, James Mlowe (katikati), akifafanua jambo kuhusu mkutano wa tisa wa wadau wa mfuko huo. Kulia ni Meneja Takwimu, Hadhari na Tathmini, Abubakar Ndwata na kushoto ni Ofisa Masoko na Mawasiliano, Rehema Mkamba.
Meneja Masoko na Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, James Mlowe (kulia), akifafanua jambo kuhusu mkutano wa tisa wa wadau wa mfuko huo. Kushoto ni Ofisa Masoko na Mawasiliano, Rehema Mkamba. 

 Meneja Masoko na Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, James Mlowe (wa pili kulia), akifafanua jambo kuhusu mkutano wa tisa wa wadau wa mfuko huo.
 Meneja Masoko na Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, James Mlowe (kulia), akifafanua jambo kuhusu mkutano wa tisa wa wadau wa mfuko huo. Kushoto ni Ofisa Masoko na Mawasiliano, Rehema Mkamba. 
 Meneja Takwimu, Hadhari na Tathmini wa Mfuko wa LAPF, Abubakar Ndwata (kulia), akifafanua jambo kuhusu mkutano wa tisa wa wadau wa mfuko huo. Kushoto ni Ofisa Masoko na Mawasiliano wa LAPF, Rehema Mkamba na katikati ni Meneja Masoko na Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, James Mlowe.

Na Mwandishi Wetu

Mfuko wa Pensheni wa LAPF unatarajia kufanya mkutano wa tisa wa wadau tarehe 9 na 10 Machi, 2017 katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa AICC Jijini Arusha. Mgeni rasmi katika mkutano huu anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb).

LAPF imekuwa ikifanya mikutano hii ili kutoa taarifa za undeshaji wa Mfuko na kuwapa fursa wadau kutoa maoni mbali mbali ili kuboresha utendaji wa Mfuko. Aidha mikutano hii hufanyika ili kutekeleza maagizo ya mamlaka ya usimamizi na udhibiti wa mifuko ya Hifadhi ya jamii nchini (SSRA).
Kauli mbiu ya mkutano wa mwaka huu ni “Kuibua Fursa Endelevu za Ajira kwa maendeleo ya Hifadhi ya Jamii Tanzania”. Pamoja na mambo mengine kwenye mkutano huu mada mbali mbali zitawasilishwa ikiwemo mada inayohusu kauli mbiu jatwa hapo juu. Mada nyingine zitahusu Utendaji wa Mfuko kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2015/2016, Taarifa ya uwekezaji pamoja na Taarifa ya Hesabu za Mfuko kwa mwaka 2015/2016.
Kadhalika katika siku ya kwanza ya ufunguzi wa mkutano LAPF  itazindua huduma ya Mkopo wa Kujikimu ijulikanayo kwa jina la Maisha Popote na LAPF) kwa kushirikiana na benki ya CRDB. Huduma hii imewanufaisha sana wanachama wa Mfuko wanaoanza ajira kwa kuwapa fursa ya kukopa mara tatu ya mshahara wao ili kukidhi mahitaji ya awali kama kulipa pango, nk kwa riba nafuu.
Vilevile siku ya ufunguzi wa mkutano tarehe 09 Machi, 2017 itakuwa ni siku ya maadhimisho ya figo duniani hivyo basi LAPF itatumia siku hii kuwapa fursa wadau wote watakao shiriki mkutano huu kupima figo kwa kushirikiana na wataalamu kutoka hospitali ya KCMC.
LAPF inatarajia kupata washiriki zaidi ya 600 katika mkutano huu kwa kuzingatia idadi ya waalikwa. Waalikwa wanaweza kuthibitisha ushiriki wao na kujisajili kwa kutembelea tovuti  ya Mfuko www.lapf.or.tz . LAPF inawahamasisha wadau wote kujisajili kupitia tovuti ili kupunguza msongamano siku ya mkutano.
Aidha, siku ya pili ya mkutano tarehe 10 Machi, 2017, LAPF pamoja na washiriki wote wa mkutano wakiongozwa na Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa wanatarajia kushiriki katika mazoezi ya kutembea ikiwa ni kuunga mkono utekelezaji wa tamko la Makamu wa Rais, Mh. Samia Suluhu Hassan.
Karibuni waalikwa wote kwa ustawi wa Mfuko.

Staafu kwa Ufahari na LAPF.

No comments:

Post a Comment

Pages