HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 18, 2017

POINTI ZA MOTO ZAITESA TFF

Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji leo imeahirisha maamuzi ya kuipoka pointi tatu na magoli matatu Simba. 


Katibu Mkuu wa TFF, Selestine Mwesigwa amesema kuwa uamuzi utatolewa Aprili 19 baada ya kuitwa na kuhojiwa ili kupata ukweli wa malalamiko ya kadi tatu za njano za mchezaji wa Kagera Sugar, Mohamed Fakhi. 


Beki wa Kagera Sugar, Mohamed Fakhi, akiwa katika viwanja vya Hoteli ya Protea jijini Dar es Salaam, wakati Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ilipoketi kupitia hukumu ya iliyowapokonya Pointi tatu Kagera Sugar.  (Picha na Francis Dande).
Makamu wa Rais wa Klabu ya Simba, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ akiwa na Mkurugenzi wa African Lyon, Rahimu Kangezi ‘Zamunda’ wakati akisuibiri maamuzi ya Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji.
Mwamuzi Jonesia Rukyaa (kushoto), akisubiri kuitwa kwa mahojiano na Kamati hiyo.
 Mohamed Fakhi (kulia), akiwa na Meneja wa Kagera Sugar, Mohamed Hussein muda mfupi kabla ya kuhojiwa na kamati.
 Meneja wa Kagera Sugar, Mohamed Hussein akifafanua jambo.
 Mohamed Fakhi 
 Kutroka kushoto ni beki wa Kagera Sugar, Mohamed Fakhi, Kocha wa makipa, Musa Mbaga na Meneja wa Kagera Sugar, Mohamed Hussein.

 Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Sheria na Uanachama wa TFFEliud Mvela akizungumza na waandishi wa habari waliofika katika Kikao cha Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji iliyokutana na kupitia hukumu ya Kagera Sugar kupokwa pointi tatu katika mchezo wao dhidi ya Simba. 
Beki wa African Lyon, Hamad Mohamed Manzi akiwa na Mohamed Fakhi.

No comments:

Post a Comment

Pages