Kaimu Mkurugenzi wa Huduma kwa Wanachama Bw. Ramadhani Mkeyenge
akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu dhana nzima ya utaratibu wa uwekaji
akiba kwa hiari kwenye Mfuko wa Pensheni wa LAPF kwenye mkutano uliofanyika Makao
makuu ya Mfuko mjini Dodoma. (Na Mpiga Picha Wetu).
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF Bw. James Mlowe akizungumza na waandishi wa Habari mjini Dodoma kuhusu umuhimu wa matumizi ya teknolojia ikiwemo huduma za M-pesa na Tigo-pesa katika kuwafikia Watanzania walio wengi ili wajiunge na kuweka akiba kupitia “LAPF Jiongeze Scheme”.
Meneja mwenye dhamana na Skimu ya
uchangiaji wa hiari (LAPF Jiongeze
Scheme) Bi. Hanim Babiker akizungumzia taratibu mbalimbali zinazotakiwa
kufuatwa ili kuweka akiba kwa njia ya M-pesa na Tigo-pesa wakati wa Mkutano na
Waandishi wa Habari mjini Dodoma.Afisa huduma kwa wanachama wanaoweka akiba
kwa hiari (LAPF Jiongeze Scheme) Bw.
Juma Venerando akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari jinsi Mfuko wa Pensheni
wa LAPF ulivyojipanga kuendelea kuboresha zaidi huduma kwa wanachama.Mwakilishi wa Kampuni ya Tigo Mkoani Dodoma Bw. Gideon Morris akizungumza na waandishi wa Habari jinsi kampuni hiyo ilivyojipanga kiteknolojia katika kuhakikisha ubora zaidi wa huduma zao za Tigo-pesa na hivyo kuwawezesha watanzania wote kuweka akiba ya hiari Kwenye Mfuko wa LAPF.
Mwakilishi wa Kampuni ya Vodacom Mkoani Dodoma Bw. Balikulije Mchome akizungumza na waandishi wa Habari jinsi kampuni hiyo ilivyojipanga kiteknolojia katika kuhakikisha ubora zaidi wa huduma zao za M-pesa na hivyo kuwawezesha watanzania wote kuweka akiba ya hiari katika Mfuko wa Pensheni wa LAPF.
Waandishi wa Habari kutoka vyombo
mbalimbali wakifuatilia kwa makini maelezo mbalimbali yaliyotolewa kwenye
utambulisho wa huduma za uwekaji wa akiba ya hiari kwa njia ya M-pesa na
Tigo-pesa kwenye Mfuko wa Pensheni wa LAPF, mkutano uliofanyika mjini Dodoma.
Safi Sana Watu WA LAPF!! Keep moving forward guys!!
ReplyDelete