Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, kuhusu maandalizi ya tamasha hilo litakalofanyika Aprili 16 kwenye Uwanja wa Uhuru. (Picha na Francis Dande).
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, kuhusu maandalizi ya tamasha hilo litakalofanyika Aprili 16 kwenye Uwanja wa Uhuru.
Na Mwandishi Wetu
ALBAMU mpya
ya ‘Jitenge na Ruth’ ya malkia wa muziki wa injili kwa uakanda wa Afrika
Mashariki na Kati, Rose Muhando, ndiyo itampandisha jukwaani katika Tamaka la
Pasaka la mwaka huu.
Muhando,
mwimbaji nguli wa nyimbo za injili nchini ambaye amekuwa akishiriki mara kwa
mara tukio hilo hata kuwa alama ya mafanikio ya muziki huo, atalitumia Tamasha
hilo kuzindua kazi hiyo mpya.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha hilo,
Alex Msama alisema albamu hiyo yenye nyimbo kibao, itazinduliwa April 16 katika
Uwanja wa Uhuru.
Msama
alisema tukio la uzinduzi wa albamu hiyo na ile ya ‘Ngome Zimeanguka’ ya
Kinondoni Revival, anaamini Tamasha la mwaka huu litakuwa tofauti.
“Malkia wa
muziki Afrika Mashariki na Kati, Rose Muhando atakuwepo katika Pasaka ya mwaka
huu akizindua albamu yake ya ‘Jitenge na Ruth,’ wadau wajitokeze kwa wingi,”
alisema Msama.
Alisema
uwepo wa Rose, Kinondoni Revial Choir, Kwa ‘Viumbe Vyote’ ya Tabora na Solly
Mahlangu kutoka Afrika Kusini na wengine mahiri, ni faraja kubwa kwa wadau wa
Tamsha hilo.
Msama
alisema, baada ya uzinduzi wa nguvu katika Uwanja wa Uhuru, siku itakayofuata
uhondo huo utahamia Uwanja wa Jamhuri, mjini Dodoma.
Alisema
wakati uzinduzi wa Uwanja wa Uhuru akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu
Mchemba atakayemwakilisha Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan, mgeni katika
Uwanja wa Jamhuri, ni Naibu wa Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavumde.
Msama
alisema baada ya Tamasha hilo kutikisa vilivyo katika Uwanja wa Jamhuri mbele ya Mavunde ambaye pia
ni Mbunge wa Dodoma mjini, litahamia katika jiji la Mwanza, Simiyu na Iringa.
Alisema
kamati yake imeamua kuufikia mji wa Dodoma kutokana na watu wake kulipenda
Tamasha hilo, pia heshima ya Dodoma kama mji mkuu wa chi na makao makuu ya serikali.
Alisema
pamoja na mambo mengine yanayokwenda na tukio hilo, malengo ya msingi ni
kueneza ujumbe wa Neno la Mungu, pia kutumia sehemu ya mapato kufariji watoto
yatima, walemavu na wajane.
No comments:
Post a Comment