Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Ineke Bussemaker,
akipata maelezo alipotembelea Taasisi ya Moyo ya Jakaya
Kikwete (JKCI) iliyopo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) jijini Dar es
Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Ineke Bussemaker, akipata maelezo alipotembelea Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) iliyopo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Prof. Mohamed Janabi.
Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Vicky Bishubo, akizungumza katika hafla hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Ineke Bussemaker, akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi miundombinu waliojenga katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) iliyopo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Ineke Bussemaker,
akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Jengo maalumu la kupumzikia wagonjwa wa nje
na wasaidizi wao wanaokwenda kupata huduma katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya
Kikwete (JKCI) iliyopo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) jijini Dar es
Salaam juzi. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa JKCI, Prof. Mohamed Janabi na Meneja
wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Vicky Bishubo.
Picha ya pamoja
NA SALUM MKANDEMBA
TAASISI ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), imeishukuru Benki ya NMB kwa kukamilisha ujenzi wa miundombinu, ikiwemo sehemu ya kupumzikia wagonjwa na ndugu wanaowasindikiza hospitalini hapo kwa matibabu.
Makabidhiano ya ujenzi huo uliogharimu Sh. Mil. 30, yalifanyika juzi nje ya jengo la JKCI, lililopo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), ambao ni sehemu ya program ya NMB ya Uwajibikaji kwa Jamii (CSR).
Akizungumza wakati wa akipokea ujenzi wa eneo hilo linaloketisha watu 100 kwa wakati mmoja, Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Profesa Mohamed Janabi, alisema ujenzi huo unaenda kukomboa mamia ya wagonjwa na wasindikizaji.
Prof. Janabi alibainsiha kuwa, eneo la kupumzikia wagonjwa na wasindikizaji ilikuwa kero kuu katika taasisi yake, ambayo inalazimisha mgonjwa mmoja kusindikizwa na watu wawili au watatu, kitu ambacho kinawafanya kupokea watu wengi.
“Kwa wastani kwa siku tunapokea watu 100 hadi 150, ambao ukijumlisha na wasindikizaji wawili au watatu, unakuta tuna jumla ya watu kati ya 300 hadi 450. Ujenzi huu ni suluhisho la msongamano uliokuwamo jengoni,” alisema Prof. Janabi.
Aliongeza kuwa, taasisi yake inajivunia misaada inayopata kutoka NMB, ambayo mwaka jana ilisaidia gharama za upasuaji wa moyo wa watoto wawili katika taasisi hiyo, ambao kwa sasa wanaendelea na masomo yao vizuri.
Prof. Janabi alisisitiza kuwa, hospitali na benki ni taasisi zinazotegemeana, kwani ili kuwa na wateja wenye afya wa huduma za kibenki, unahitaji huduma bora za kimatibabu, ikiwemo miundombinu na vifaa tiba.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Ineke Bussemaker, alisema ushirikiano wao na jamii ni moja ya vipaumbele vya NMB na kwamba wanajisikia faraja kufanikisha utatuzi wa changamoto za jamii, ukiwemo ujenzi huo, Bussemaker aliongeza kuwa, NMB imetenga zaidi ya Sh. Bil. 1 kwa mwaka 2017, zitakazosaidia katika Sekta ya Afya, Elimu na usaidizi wa majanga ya kijamii na kuwa mwaka jana walitumia zaidi ya Sh. 260 kwa hospitali 33 nchini.
No comments:
Post a Comment