Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la wenye Viwanda Tanzania (CTI), Leodegar Tenga, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa hafla ya kusaini mkataba wa udhamini wa Tuzo za Rais za Mzalishaji Bora wa mwaka viwandani zitakazofanyika Aprili 8 jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Benki M, Jacqueline Woiso.
Mkurugenzi Mkuu wa Benki M, Jacqueline Woiso (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa hafla ya kusaini mkataba wa udhamini wa Tuzo za Rais za Mzalishaji Bora wa mwaka viwandani zitakazofanyika Aprili 8 jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Benki M, Jacqueline Woiso (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa hafla ya kusaini mkataba wa udhamini wa Tuzo za Rais za Mzalishaji Bora wa mwaka viwandani zitakazofanyika Aprili 8 jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Benki M, Jacqueline Woiso (kushoto), akisaini leo mkataba na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la wenye Viwanda Tanzania (CTI), Leodegar Tenga, kwa ajili ya udhamini wa Tuzo za Rais za Mzalishaji Bora wa mwaka viwandani zitakazofanyika Aprili 8 jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Benki M, Jacqueline Woiso (kushoto), akisaini leo akibadilishana mkataba na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la wenye Viwanda Tanzania (CTI), Leodegar Tenga, wa udhamini wa Tuzo za Rais za Mzalishaji Bora wa mwaka viwandani zitakazofanyika Aprili 8 jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi Wetu
Tuzo za Raisi za
mzalishaji bora wa mwaka viwandani 2016 zitatolewa tarehe 8 Aprili mwaka 2017 katika ukumbi wa hoteli ya Serena
jijini Dar es salaam. Benki M kwa mwaka wa pili mfululizo ndiye mdhamini mkuu
wa tuzo hizo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa shirikisho la viwanda Tanzania (CTI) Leodegar Tenga alisema kuwa tuzo hizo zinalenga kutambua na
kuthamini mchango mkubwa unaotolewa na sekta ya viwanda nchini katika kukuza
uchumi.
Amesema kuwa kwa
takribani miaka kumi na mbili mfululizo, shirikisho hili limekuwa likitoa tuzo
hizo kubwa kwa wanachama wake ambao hujumuisha sekta zote za uzalishaji na
huduma.
Shindano la mwaka
huu limeboreshwa zaidi kwa kuingiza katika shindano zawadi ya matumizi bora ya
Nishati. Zawadi hii pia itasaidia kuhamasisha washiriki kuhusu umuhimu wa
kufanya kazi kwa kuzingatia matumizi bora ya nishati viwandani. CTI, DANIDA na
GIZ zimekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha usimamizi na matumizi bora ya
nishati viwandani mfano, ukaguzi wa nishati viwandani uliofanywa na unaoendelea
kufanywa nchini kote kwa wananachama wa CTI.
Na kwa mara ya
kwanza, shindano la mwaka huu pia litashirikisha kampuni zisizo wanachama wa
shirikisho hilo. “Ili kutekeleza ushauri alioutoa Mh. John Pombe Magufuli, Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye pia ni Mlezi wa CTI, katika hafla ya
kukabidhi tuzo kwa washindi mwaka jana, CTI imeamua kupanua wigo wa ushiriki
kwa kualika Kampuni zisizo wanachama kushiriki ili kulifanya shindano kuwa la
kiushindani zaidi” alisema.
Dhumuni kuu la
tuzo hizi ni kutambua mchango wa sekta ya viwanda katika ukuaji wa uchumi,
kuwavutia wawekezaji zaidi katika sekta ya viwanda, kutangaza umuhimu wa sekta
ya viwanda nchini, kukuza kiwango cha biashara nk.
Bw. Tenga alitoa
shukrani zake za dhati kwa Benki M kwa kushirikiana nao kama wadhamini wakuu wa
tuzo hizo kwa mwaka wa pili mfululizo.
Kwa upande wa
Benki M, Mkurugenzi Mkuu wa Benki hiyo Bi. Jacqueline Woiso alisema kuwa Benki M inatambua juhudi za serikali katika kuinua
sekta ya viwanda nchini.
“Sekta ya viwanda ni sekta muhimu sana katika kukuza uchumi hivyo tunajisikia fahari kusaidia wazalishaji wa viwanda wa ndani siyo kifedha au kuwapatia huduma za kibenki tu lakini pia kupitia shindano hili maarufu la thamani. Tuzo za mzalishaji bora ni mahali ambapo makampuni wanachama na wasio waachama wa CTI kupitia mchakato wa ushindani huinua ubora wa bidhaa wanazozalisha na huduma wanazotoa katika jamii” alisema Bi Woiso.
“Sekta ya viwanda ni sekta muhimu sana katika kukuza uchumi hivyo tunajisikia fahari kusaidia wazalishaji wa viwanda wa ndani siyo kifedha au kuwapatia huduma za kibenki tu lakini pia kupitia shindano hili maarufu la thamani. Tuzo za mzalishaji bora ni mahali ambapo makampuni wanachama na wasio waachama wa CTI kupitia mchakato wa ushindani huinua ubora wa bidhaa wanazozalisha na huduma wanazotoa katika jamii” alisema Bi Woiso.
Tuzo za raisi za
mzalishaji bora wa mwaka zilianza kutolewa mwaka 2005, ni tuzo ambazo
huandaliwa na shirikisho la viwanda Tanzania (CTI) katika kutambua mchango wa
sekta ya uzalishaji wa viwanda nchini.
Mwishoni wa
mchakato wa kupata washindi, walioshinda hupewa tuzo na mheshimiwa Raisi wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ndiye mlezi wa Shirikisho hilo. Kwa
mwaka huu, Mheshimiwa Rais atawakilishwa na Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan.
Tuzo hizi hutolewa
kwa makampuni na viwanda kuanzia vidogo, vya kati hadi vikubwa kutegemea
mchango vinaotoa katika kukuza uchumi nchini. Mwaka huu hafla hii inatarajiwa
kuhudhuriwa na wadau mbalimbali Takribani 400 wakiwamo wafanyabiashara wakubwa
na wadogo, wenye viwanda na wataalamu mbalimbali na waalikwa kutoka katika
sekta binafsi na serikali.
No comments:
Post a Comment