Ameyasema hayo baada ya kuzungukia maeneo yote ya shule
yanayoendelea kukarabatiwa wakati alipofanya ziara ya kushtukiza ili kujionea
hatua waliyofikia katika ujenzi na kutathmini kama thamani ya pesa inakwenda
sambamba na ujenzi unaoendelea katika shule hiyo.
Shule ya Sekondari ya Kantalamba ni miongoni mwa shule
kongwe 20 nchini ambazo serikali kupitia Wizara ya Elimu imeweka mpango wa
kukarabati shule hizo kwa lengo la kutunza hadhi na kuziboresha zaidi. Ambapo shule
hiyo imepata mgawo wa shilingi 1,123,353,700/=
“Tafadhalini sana Mwalimu Mkuu, Mkurugenzi, Afisa Elimu na
sisi wote tuhakikishe kwamba shule hii imebadilika kwa kuwa hizi pesa si
kidogo, bilioni sio hela kidogo, zisichezewe, zifanye kazi iliyokususdiwa na
kazi yenyewe ioneshe sura ya bilioni, isijekutokea tukapata kazi nyingine ya
kusema kwamba hizi pesa kazi iliyofanyika ni ya hovyo hovyo,” Mh. Zelote
Alisisitiza.
Baada ya kuona juhudi zinazoendelea katika ukatabati huo Mh.
Zelote amesifu uongozi wa shule wa kuajiri mafundi vijana waliopo mtaani ili
kuwa na matumizi mazuri ya fedha hizo tofauti na kuwatumia wakandarasi ambao
wangesababisha fedha nyingine zipotee bila ya sababu, na kusisitiza kuwa vijana
hao wasimamiwe kwa ukaribu sana na kupewa maelekezo ili wasilipue kazi
inayoendelea.
Pamoja na hayo Mh. Zelote alilisisitiza uwazi kwenye
matumizi ya fedha za umma, na kuwataka wakaguzi kuwa makini na kukagua kila
hatua ya ujenzi na kuona kuwa kila senti inayotumika inaendana na thamani ya
ujenzi inayoonekana
Aidha alizitaka Halmashauri zote Mkoani Rukwa kutenga bajeti
kwa kupitia mapato yake ya ndani ili
kuboresha miundombinu ya shule jambo ambalo linaweza kubadilisha muonekano wa
shule nyingi mkoani humo.
“Ningependa kuona shule hii inakuwa ya mfano kwakuwa ipo
katika makao makuu ya mkoa na pia alishauri kujenga uzio na kuendeleza utunzaji
wa mazingira kwa kuweka sharia kali kwa wanafunzi ili waendelee kutunza
mazingira ya shule,” Mh. Zelote aliongezea.
Awali alipokuwa akisoma taarifa fupi ya ukarabati wa shule
kongwe Sekondari ya Kantalamba mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Martin Kasansa alitaja
changamoto kadhaa zinazorudisha nyuma kasi ya ukarabati wa shule hiyo ikiwemo
uchakavu mkubwa wa bwalo uliosababisha kuanza upya ujenzi, upatikanaji wa
baadhi ya vifaa mkoani Rukwa kuwa mgumu na kulazimika kuagiza kutoka mkoa wa Mbeya
na kutopatikana kwa maji kumechelewesha ujenzi unaoendelea.
“Kazi ya ukarabati ilianza rasmi mwezi June 2017 na
inasimamiwa na mwandisi kutoka Chuo cha Sayansi na teknolojia Mbeya na
inategemewa kumalika ndani ya miezi mitatu, lakini upatikanaji wa maji umekuwa
ni tatizo katika eneo letu, ” Martin Alisema
Ukarabati unaoendelea katika shule hiyo unahusisha mabweni
6, vyumba vya madarasa 14, ofisi za walimu, vyoo, mfumo wa maji safi na maji
taka, mfumo wa umeme, jiko, bwalo, maabara pamoja na jingo la kilimo. Ambapo mapaka
sasa Shilingi 648,051,540.90/= imeshatumika na kufikia asilimia Zaidi ya 58.
Nae Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa Bernard Makali aliutaka
uongozi wa shule kuangalia maeneo muhimu na kuweaza kuyamalizia ili wanafunzi
wasiachwe nyuma na muhula wa mwaka huu na kusisitiza kuwa upishi wa kutumia
kuni si mzuri na kuahidi kushikiana nao kutafuta namna ya kupikia kwa kutumia
gesi jambo ambalo litatunza mazingira.
No comments:
Post a Comment