HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 18, 2017

TADB yavutiwa na Kiwanda cha Chobo

Na mwandishi Wetu, Mwanza

Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imesema imeridhishwa na uwekezaji wa Kiwanda cha Nyama cha Chobo kilichombo Misungwi jijini Mwanza kwa kuwa kinawahakikishia wakulima wadogo masoko ya mifugo yao.

Pongezi hizo zimetolewa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga wakati alipofanya ziara ya kujionea maendeleo ya uwekezaji wa miundombinu ya Kiwanda hicho.

Bw. Assenga amesema kuwa Kiwanda cha Chobo ambayo inamilikiwa na kijana mzalendo, John Chobo ina uwezo mkubwa wa kusadia wakulima wadogo kwa kununua mifugo yako hivyo kuwapatia fursa za masoko wakulima hao.

“Miundombinu ya Kiwanda inaweza kuchinja zaidi ya ng’ombe 600 kwa siku, hili ni soko kubwa sana kwa wakulima wadogo wa mikoa ya Kanda ya Ziwa hali itakayounga mkono juhudi za serikali hasa TADB katika kuboresha minyororo ya thamani kwenye sekta ya mifugo,” alisema.

Bw. Assenga amesema Serikali iliamua kuanzisha Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) ili kusaidia kukabiliana na mapungufu ya wakulima nchini kote ili kuhuisha upatikanaji wa mikopo katika sekta ya kilimo na kuchagiza mapinduzi katika kilimo nchini.

Bw. Assenga ameongeza kuwa sekta ya mifugo ni mojawapo ya minyororo ya mwanzo inayopatiwa mikopo kwa ajili ya uongezaji wa thamani mazao na mifugo mbalimbali hasa katika uongezaji wa thamani wa ufugaji wa ng’ombe wa nyama na maziwa nchini.

Ameongeza kuwa Benki yake imejipanga kuendeleza uongezaji wa thamani wa Ufugaji wa Ng’ombe wa Nyama na Maziwa.

“Benki inatoa mikopo na kusaidia uwekezaji kwa ajili ya ujenzi, ununuzi wa mitambo na ufungaji wa mitambo ya kuhudumia ng’ombe ikiwemo majosho na mabwawa ya kunyweshea na pamoja na usindikaji wa nyama na maziwa kwa ajili ya kuongeza thamani nyama na maziwa,” alisema Bw. Assenga. 

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mmiliki wa Kiwanda hicho, Bw. John Chobo alisema kuwa kwa sasa kiwanda chake hakijafikia uwezo wa kutumika kwa asilimia 100 kutokana na changamoto za kimtaji zinazomkabili na alitumia fursa hiyo kuiomba Benki ya Kilimo kumuwezesha ili aweze kutoa ajira zaidi kwa Watanzania.

Kwa mujibu wa Bw. Chobo kwa sasa kiwanda chake kina wafanyakazi 85 na kikifikia uwezo wa kuzalisha kwa asilimia 100 kitaweza kuajiri zaidi ya wafanyakazi 300 watakaofanya kazi kiwandani na 300 watakaokuwa wakisimamia shamba.

“Tunaiomba TADB kutatulia changamoto za ukosefu wa mitaji ya uhakika kwa kuwa kwa kiasi kikubwa na mikopo mingi kutoka taasisi za fedha kuelekezwa zaidi kwenye upande wa biashara za bidhaa na ambayo riba yake ni kubwa sana.,” alisema.

No comments:

Post a Comment

Pages