Mwenyekiti
wa Kamati ya Tiba ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Dkt.
Paul Marealle ameitisha kikao cha Kamati ya Tiba kitakachofanyika kesho
Jumatano Agosti 30, mwaka huu kuanzia saa 4:00 asubuhi.
Kikao
hicho kitakachofanyika Ukumbi wa Ofisi za Makao Makuu TFF, yaliyoko
Uwanja wa Kumbukumbu ya Uwanja wa Karume, Ilala jijini Dar es Salaam
kitarejea shughuli zake kwa mujibu wa Katiba ya TFF sambamba na Kanuni
zinazoongoza mashindano mbalimbali ya TFF.
Katika
kikao hicho, pia kamati itapitia fomu za afya za utimamu wa mwili za
wachezaji wote wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL); Ligi Daraja
la Kwanza (FDL) na Ligi Daraja la Pili (SDL).
Miongoni
mwa majukumu ya kamati hiyo ni kupitisha wachezaji wanaopaswa
kucheza/kushiriki katika ligi baada ya kujirisha juu ya utimamu wa mwili
wa wachezaji kwa michuano tajwa hapo juu.
KAMATI YA NIDHAMU KUKETI KESHO
Kamati
ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), chini ya
Mwenyekiti wake Tarimba Abbas, kinatarajiwa kuketi kesho Jumatato Agosti
30, mwaka huu.
Kamati hiyo itakuwa na ajenda kadhaa ikiwamo ya mashauri yanayohusu wachezaji mbalimbali, viongozi na klabu.
Kwa taarifa zaidi, fuata link hapo chini
……………………………………………………………………..…… ………..……
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA
No comments:
Post a Comment