HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 19, 2017

Asasi za kijamii zinapunguza uhaba wa ajira

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamis Kigwangalla akifungua mkutano mkutano wa kuzijengea uwezo asasi za kijamii jijini Dar es Salam.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamis Kigwangalla (kulia) akipokea tuzo kutoka kwa Mwenyekiti wa Asasi ya An-Nahl Trust, Mhandisi Alliy Kiloma, baada ya kufungua mkutano wa kuzijengea uwezo asasi za kijamii jijini Dar es Salam. Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa An-Nahl Trust, Musa Nyamsigwa. (Picha na Francis Dande).  

NA MWANDISHI WETU


IMEELEZWA kwamba asasi za kijamii zinaisaidia serikali kupunguza tatizo la ajira kwa kuwahamasisha vijana kuwa wajasiriamali.

Akizungumza katika mkutano wa uwekezaji wa asasi za kijamii, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Wtato, Dk. Hamis Kigwangalla, alisema kwamba asasi za kijamii zina mguso wa haraka kwa jamii lengwa kwa sababu zinakuwa karibu na walengwa hali inayosaidia kuondoa changamoto kwa wakati.


Alisema kwamba sifa ya asasi za jamii ni kwamba haziendeshi shughuli zake kwaajili ya kupata faida bali kwa kutokana na dira, dhamira na maslahi ya umma.


Naye Ofisa Mtendaji Mkuu wa An Nahl Trust, Musa Nyamsigwa alisema kwamba lengo la kukutana kwao ni kukuza asasi za kijamii ili kupata mafunzo ya namna bora ya kuziendesha na kuwafanya vijana kuwa na mchango mkubwa katika jamii.


“Kuna mafunzo maalum yamefanyika ambayo yakitumika yatasaidia jamii, asasi ili kuwaelekeza hatua bora za utendaji wao na kupata ufanisi bora na utawala uliotukuka.

No comments:

Post a Comment

Pages