Wabunge
wa zamani wa majimbo ya Nachingwea na Lilundi, Mhe. Maokola Majogo (kulia)
na Anna Abdallah wakipata maelezo mbalimbali ya Kiwanja cha Ndege cha
Mtwara, kutoka kwa Mhandisi Kedrick Chawe na Bi. Harieth Nyalusi katika
maonesho yanayokwenda sambamba na Kongamano la Kwanza la Kitaifa la
Usafiri wa Anga, lililomalizika leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa
wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam.
Bw. Geoffrey Tupper (kulia) akikusanya makabrasha mbalimbali yanayotoa
maelezo ya viwanja vya ndege kutoka katika meza ya maonesho ya Mamlaka ya
Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), yaliyokuwa yakienda sambamba na
Kongamano Kwanza la Kitaifa la
Usafiri wa Anga, lililomalizika leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa
wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Bi. Fatma Matimba na
Mhandisi Kedrick Chawe wa TAA.
Mhandisi Kedrick Chawe akimfafanulia masuala mbalimbali ya Viwanja vya
ndege, Bi. Mwamini Mohamed aliyetaka kujua ujenzi wa jengo la Tatu la
abiria la Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TBIII),
wakati wa Kongamano la Kwanza la Kitaifa la Usafiri wa Anga lililomalizika
leo kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
Kaimu Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere
(JNIA), Bw. Johannes Munanka akichangia mada kwenye Kongamano la siku
mbili la Kwanza la Kitaifa la Usafiri wa Anga, lililomalizika leo kwenye
ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) (wa tatu
kutoka kushoto), Bw. Salim Msangi akihudumia wananchi waliofika kutaka
maelezo mbalimbali kwenye meza ya maonesho ya TAA yaliyokwenda sambamba na
Kongamano la Kwanza la Kitaifa la Usafiri wa Anga lililomalizika leo
kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es
Salaam. Wengine kuanzia kulia ni Mhandisi Kedrick Chawe, Bi. Harieth
Nyalusi na Bi. Rose Comino wa TAA.
No comments:
Post a Comment