HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 25, 2017

NYOTA WA ZAMANI YANGA ATUHUMIWA KUTAKA KUDHULUMU NYUMBA YA URITHI

NA SHEHE SEMTAWA

FAMILIA ya Mabrouk imemripoti mchezaji wa zamani wa timu ya Yanga na Simba, Athuman China Kituo cha Polisi Urafiki, ikimtuhumu kutishia usalama wa watoto wa dada yake ambao wako katika mgogoro wa kugombea nyumba.

Mahamuod Mabrouk, ameyasema hayo baada ya kubaini kuwa tangu ulipozuka mgogoro huo kumezuka tabia ya baadhi ya watu wasiojulika wamekuwa wakifika nyumbani hapo wakiwa na mjomba wao (China) bila sababu za msingi.

Nyumba hiyo namba 123 ipo Sinza kwa Madukani mtaa wa Chimwaga, jijini Dar es Salaam.

Watoto ambao ni Aziz na Mahamoud wanadai kuwa mjomba wao huyo anataka kuwadhulumu nyumba akishirikiana na mama yao mdogo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam juzi, Mabrouk, alisema kuonekana watu hao nyumbani kwao kunawatia hofu hivyo kuwafanya waishi kwa wasiwasi.

Alisema amechukua uamuzi huo kwa ajili ya usaalama wa familia yake, endapo kutatokea tatizo basi polisi watajua wanaanzia wapi uchunguzi wao.

"Kweli nilikwenda kutoa taarifa katika kituo hicho cha Polisi Urafiki na kufungua jalada ambalo ni URP/RB/8799/17, (Urafiki kujihusisha na waharifu dhidi ya watoto wa dada yake, kwenye nyumba iliyo na kesi mahakamani)," alisema Mahamuod

Hata hivyo, Mahamuod, alisema hawezi kuzungumzia kwa undani mgogoro huo unaoihusu nyumba kwa vile kuna kesi ya msingi Mahakamani.

Alipotafutwa China ili kuthibitisha kama taarifa hizo ni za kweli, alisema, hadi anazungumza na mwandishi, alikuwa hana taarifa kuhusu RB hiyo.

"Kwani umefanyika uhalifu? Sasa mimi nisifike pale wakati pale ni nyumbani kwetu? Mimi nitafika tu, tena bila kipingamizi chochote," alisisitiza China.

Aliongeza kuwa: "Kuhusu shauri lililoko mahakamani ni kweli lipo, kwamba nilifungua kesi ya kuwataka watoto hao waondoke kwenye nyumba ya mzee.

"Hata hivyo, familia hiyo nayo ilikwenda mahakamani kuweka pingamizi kwa madai kuwa nyumba hiyo imejengwa na mama yao katika kiwanja hicho kwa makubaliano ya familia ya Mzee Chabwa," alifafanua.

No comments:

Post a Comment

Pages