Wananchi wa Mkoa wa Rukwa wameshauriwa kuweka utamaduni wa
kugfanya mazoezi kila siku kwa lengo la kuyaenzi Maisha ya Hayati Baba wa Taifa,
kwani kufanya hivyo ni kwa faida ya afya zetu wenyewe.
Yamesemwa hayo na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu
Zelote Stephen katika kuadhimisha kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu
Julius Nyerere katika kiwanja wa Nelson Mandela, mjini Sumbawanga.
Maadhimisho hayo yaliyokwenda sambamba na jumamosi ya pili
ya mazoezi pamoja na kilele cha wiki ya vijana wananchi walijitokeza kwa wingi
asubuhi kwaajili ya kushiriki kwenye mbio zilizoanza ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa
Rukwa na kuelekea kwenye jkiwanja hicho cha mpira kikubwa mkoani Rukwa.
Amesema kuwa watanzania wameacha kufanya mazoezi hali
inayopelekea kunyemelewa na magonjwa mbalimbali hali inayopelekea kupunguza
nguvu kazi ya taifa.
Ameongeza kuwa Katika kuiweka afya yake vizuri, hutumia
dakika 20 asubuhi kufanya mazoezi kabla ya kuelekea ofisini hali iliyopelekea
kuoneka na afya nzuri mbali na kuwa na umri mkubwa.
“Msinione bado nipo fiti ni kwasababu ya kufanya mazoezi
kila siku kwa dakika 20 kabla sijaingia ofisini, mazoezi haya ni faida yetu
wenyewewe, sio faida ya Rais, Makamu wa Rais wala Waziri Mkuu, na Katika kuona
kuwa watanzania wameacha mazoezi Serikali ya ikaagiza kila jumamosi ya pili ya
mwezi iwe ya mazoezi si kwasababu nyingine bali ni kuendelea kutunza afya zetu,”
Alifafanua.
Pia alitumia nafasi hiyo kumuagiza Katibu Tawala wa Mkoawa
Rukwa kuhakikisha kuwa anaweka utaratibu wa kuhakikisha kila mtumishi wa
serikali anashiriki kwenye mazoezi hayo ili kuimarisha afya zao na kuendeleza
kulijenga taifa.
Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa Bernard Makali
katika kuisemea kilelel cha wiki ya vijana, amewataka vijana wote mkoani humo
kuandika maoni juu ya fani watakazotaka zifundishwe katika chuo kipya cha
ufundi VETA kinachotarajiwa kuanza kujengwa katika makao makuu ya Mkoa huoMjini
Sumbawanga.
“Katika kuhakikisha huduma mbalimbali za kiufundi zinapatika
katika Mkoa wetu, hivi karibuni serikali itaanza kujenga chuoi cha ufundi VETA
cha kisasa kabisa, hivyo make tayari kwa hilo na wamekuja kutaka kutaka maoni
juu ya fani ambazo tunataka zifundishwe kwenye chuo hivyo ni fursa yenbu kuleta
maoni ya fani mnazotaka zifundiswe kwenye chuo hicho,” Alimalizia.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Kamishna Mstaafu Zelote Stephen (kulia), akipimwa macho zoezi lililoendeshwa kwa wananchi wote
waliohudhuria katika maadhimisho ya kifo baba wa Taifa, Kiwanja cha Mandela,
Mjini Sumbawanga, baadaya kupima alionekana hana tatizo.
No comments:
Post a Comment