Daktari wa Mifugo na Kilimo, Dk. Aloyce Kessy, akitoa mafunzo ya jinsi ya kuandaa vitalu vya miche ya papai katika kikao cha mpango kazi kwa watalaamu wa kilimo wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (MKIKITA) watakaokuwa wanasimamia mashamba makubwa yaliyoanzishwa na mtandao huo maeneo ya Ruaha mkoani Iringa, Kibaha na Vikindu mkoani Pwani. Kikao hicho kimefanyika leo eneo la Goba, Dar es Salaam. (Picha na Richard Mwaikenda).
Dk. Kessy akifafanua jambo wakati wa kikao hicho. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mkikita, Adam Ngamange, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mtandao huo, Dk. Kissui S Kissui na Mkurugenzi wa Miradi na Maendeleo ya Biashara wa Mkikita, Edwin Mkwanga
Washiriki wakisikiliza kwa makini wakati Dk. Kessy akitoa mafunzo hayo
Mkurugenzi Mtendaji wa Mkikita, Adam Ngamange akiwaelea watalaaamu hao kuhusu majukumu yao.
Watalaamu wa kilimo wa Mkikita wakiwa makini kusikiliza maelekezo ya jinsi ya kuboresha kilimo cha papai.
No comments:
Post a Comment