HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 16, 2017

Dk. Shein Mgeni rasmi mkutano na utoaji wa Tuzo za Pan African Humanitarian Summit

NA TATU MOHAMED

RAIS na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Zanzibar, Dk. Ally Mohammed Shein anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi katika mkutano na utoaji wa Tuzo za Pan African Humanitarian Summit.

Mkutano na utoji wa Tuzo hizo zenye lengo la kutambua jitihada mbalimbali zinazofanywa na wadau barani Afrika ili kuendeleza na kudumisha diplomasia na amani utafanyika Novemba 18 mwaka huu jijini Dar es salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam jana, Mratibu wa mkutano huo kutoka Asasi ya Vijana wa umoja wa Mataifa (YUNA), Selemani Kitenge, amesema mkutano huo utatoa fursa kwa watu mbalimbali wakiwamo Watu mashuhuri kutoka nchi tofauti barani Afrika kujadili mustakabali wa diplomasia na amani.

"Kwa upande wa  tuzo pamoja na vipengele vingi lakini kuna viwili muhimu ambavyo ni pamoja na cha Rafiki wa Afrika ambacho ni mahsusi watu walio nje ya Afrika ambao wamekuwa mchango mkubwa katika masuala mbalimbali barani hapa.

"Kipengele cha pili ni Peace Building (Mlinda amani) tuzo ambayo itatolewa watu ambao wamefanya vizuri katika kuhamasisha amani na diplomasia," amesema.

Ameongeza kuwa mkutano huo utawaleta pamoja wanadiplomasia, wadau wa maendeleo pamoja na vijana madhubuti kutokana  katika nyaja mbalimbali barani Afrika,viongozi wa serikali.

Kitenge amesema dhima ya mkutano huo kwa mwaka huu ni Amani inawezekana Jana,sasa na kesho.
Aidha amesema tuzo hizo zilianza kutolewa toka mwaka 2015 ambapo Tanzania ni nchi ya pili kuandaa mkutano huo.

No comments:

Post a Comment

Pages