Mkuu wa Kitengo cha Ulinzi na Usalama
cha Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Lugano
Mwansasu (kulia), akitoa maelezo kwa Maafisa wa Idara mbalimbali kutoka
kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Abeid Amani Karume cha Zanzibar
(AAKIA) waliofanya ziara ya mafunzo. Kushoto ni Msaidizi wa Mkuu wa
kitengo cha Ulinzi na usalama JNIA, Bw. Hamis Mashaka.
Maafisa
wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Abeid Amani Karume cha Zanzibar
(AAKIA), Bw. Shaaban Kombo (kuanzia wa pili kulia), Bi. Zakhia Mohamed,
Bw. Salehe Said na Bi. Fatma Yussuf wakimsikiliza Mkuu wa Kitengo cha
Ulinzi na Usalama cha Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere
(JNIA), Bw. Lugano Mwansasu (kulia) akiwaelekeza jambo wakati wa ziara yao
ya mafunzo iliyofanyika leo.
Msaidizi wa Mkuu wa Kitengo cha Ulinzi
na Usalama wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA),
Bw. Hamis Mashaka (kushoto), akitoa maelezo mbalimbali yanayohusiana na
ulinzi na usalama kwa maafisa kutoka idara mbalimbali za Kiwanja cha Ndege
cha Kimataifa cha Abeid Amani Karume (AAKIA) cha Zanzibar walipofanya
ziara ya mafunzo leo.
Meneja Uendeshaji cha Kiwanja cha
Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Vedastus Fabian (kulia)
akiwapa maelezo mbalimbali Maafisa kutoka Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa
cha Abeid Amani Karume (AAKIA) walipofanya ziara ya mafunzo leo.
Afisa Habari katika jengo la Watu Mashuhuri la Kiwanja cha Ndege cha
Kimataifa cha Julius Nyerere (VIP-JNIA), Bw. Kenny Kwenga (kushoto) akitoa
maelezo ya namna watu mashuhuri wanavyohudumiwa kwa maafisa kutoka Kiwanja
cha Ndege cha Kimataifa cha Abeid Amani Karume (AAKIA), walipofanya ziara
leo. Kulia ni Msimamizi wa VIP, Bi. Josephine Mwaisukule.
No comments:
Post a Comment