HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 19, 2017

NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI ATEMBELEA SHIRIKA LA POSTA

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (wa pili kulia), akimsikiliza Kaimu Postamasta Mkuu wa TPC, Hassan Mwangombe, wakati akimpatia maelezo kuhusu shirika hilo, katika ziara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. 
Kaimu Postamasta Mkuu, Hassan Mwangombe (kushoto), akimweleza jambo Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye, wakati akikagua mabasi mapya ya usafirishaji abiria na vifurushi.   
Kaimu Postamasta Mkuu, Hassan Mwangombe (kushoto), akimpatia maelezo Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (katikati), kuhusu vifurushi vinavyotumwa na kupokelewa kutoka nje ya nchi.
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (katikati), akipatiwa maelezo na mmoja wa wakaguzi wa vifurushi vinavyotumwa nje ya nchi, alipofika kitengo cha kuhudumia vifurushi, Posta Kuu jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa wateja wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Dk. Louis Shika, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu huduma za shirika, alipokutwa na waandishi katika ziara ya Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye. 
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye, akipatiwa maelezo na mmoja wa wafanyakazi wa Posta Kuu, Kitengo cha EMS, Sanjile Mbano (kulia), alipofika kwenye kitengo hicho, katika ziara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. 
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (katikati), akipatiwa maelezo na Meneja wa Idara ya EMS, John Tinga.
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye, akizungumza na wafanyakazi wa Posta Makao Makuu na wa Mkoa wa Dar es Salaam alipokutana nao katika ziara hiyo.
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania (TEWUTA-TPC), Makao Makuu, Ahmed Kaumu, akimuuliza swali Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye katika mkutano huo.

No comments:

Post a Comment

Pages