SHIRIKA lisilo la Kiserikali la Coconut Foundtion lenye Makao yake Makuu Kijitonyama Manispaa ya Kinondoni jijini Dar-es-Salaam, leo hii limewatangaza washindi kumi baada ya kumalizika kwa shindano la kutaja herufi sahihi ya sentensi za kiingereza, lililoanza Novemba 11.
Wahusika wa shindano hilo, walikuwa wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari (English Medium School). Shindano hilo lilikuwa na lengo la kuwajengea uwezo na kujiamini katika matumizi ya lugha ya Kiingereza.
Washindi hao wanatarajia kwenda kwenye mashindano hayo nchini Uganda mnamo mwezi Desemba mwaka huu, ambako mashindano hayo yatazijumuisha nchi za Afrika Mashariki.
Shirika la Posta Tanzania lilikuwa miongoni mwa wafadhili wa shindano hilo.
Afisa Masoko wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Maria Sanga (katikati), akiwa na baadhi ya washiriki wa shindano la Spelling Bee pamoja na mwalimu wao baada ya kutembelea meza ya Shirika la Posta Tanzani na kupewa zawadi mbalimbali ikiwepo kofia.
Afisa Masoko Mwandamizi wa Shirika la Posta Tanzania, Bw. Phillip Kowero, akifunga rasmi shindano la Spelling Bee lililomalizika Novemba 18 katika ukumbi wa jumba la Makumbusho ya Taifa, ambapo Shirika la Posta Tanzania wakiwa ni moja kati wadhamini wa shindano hilo.
Afisa Masoko Mwandamizi wa Shirika la Posta Tanzania, Bw. Philip Kowero akimkabidhi cheti Mwalimu wa kutoka Shule ya Feza baada ya shule yao, kufanya vizuri katika shindano hilo.
Walimu kutoka Shule mbalimbali na wazazi wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washindi wa shindano la National Spelling Bee, lililofanyika katika ukumbi wa jumba la Makumbusho jijini Dar-es-Salaam.
Washindi wa shindano la National Spelling Bee wakiwa katika picha ya pamoja, mara baada ya kumalizika kwa shindano hilo.
No comments:
Post a Comment