HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 20, 2017

NLUPC YAANZA KUREJEA MWONGOZO WA UPANGAJI MATUMIZI YA ARDHI YA WILAYA

 Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi (NLUPC) Dkt. Stephen Nindi akielezea kwa ufupi malengo ya warsha kwa ajili ya kurejea mwongozo wa upangaji,utekelezaji na usimamizi wa mipango ya matumizi ya ardhi ya Wilaya, Mjini Morogoro
 Kaimu Mkurugenzi wa Uratibu, Sera na Mawasiliano wa Tume Bi. Albina Burra akitoa maelezo mafupi kwa Mkurugenzi wa NLUPC Dkt. Stephen Nindi kuhusiana na kazi ya kurejea mwongozo wa upangaji,utekelezaji na usimamizi wa mipango ya matumizi ya ardhi ya Wilaya.

Tume na wadau mbalimbali  kutoka Serikalini, Asasi za kiraia wamekutana Morogoro kwa ajili ya kutengeneza urejewa mwongozo wa upangaji,utekelezaji na usimamizi wa mipango ya matumizi ya Ardhi ya Wilaya.

Akizungumza wakati wa mchakato huo Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya mipango na Matumizi ya Ardhi (NLUPC) Dkt. Stephen Nindi alisema kuwa NLUPC  ikishirikiana na Haki Ardhi pamoja na wadau mbalimbali wanaojihusisha na upangaji, utekelezaji  wa usimamizi wa mipango ya ardhi wamekutana kwa ajili ya kuanza kupitia namna ya upangaji wa matumizi ya Ardhi ya Wilaya ambapo mwongozo huo uliandaliwa tangu mwaka 2006.

“Kutokana na mambo mengi  kutokea kwa muda wa miaka kumi na moja (11), ambayo tungependa  yawepo katika muongozo huu wa namna ya kuandaa mipango ya matumizi ya ardhi ya Wilaya, mambo hayo yaliyojitokeza ni kama mabadiliko ya tabianchi na athari zake kuwa kubwa inayopelekea mabadiliko ya hali ya kimazingira, ushirikishwaji wa jinsia pamoja na makundi mengine madogo madogo mfano watu wanaotegemea mizizi na wanaohama hama toka sehemu moja kwenda sehemu nyengine” Alisema Dkt. Nindi.

Aliongeza kuwa  Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt John Pombe Magufuli anayesisitiza kuwa  Nchi iwe  ya viwanda na uchumi wa kati, na katika muongozo wa kuandaa mpango wa  matumizi ya ardhi ya Wilaya haukuupa msukumo wa viwanda. Mwongozo huu utaangalia utaratibu wa  namna gani  viwanda vitaendelea katika ardhi ya Wilaya na vijiji.

Kutokana na mabadiliko mbalimbali yaliyotokea nchini yakiwomo ya kiuchumi,kisiasa,kijamii,na ndani ya miaka hii kumi na moja kumekuwa na ukuaji wa mashamba ya saizi ya kati ekali 100 hadi 150 umeongezeka ambapo unahitaji muongozo mpya na namna ya kusimamia katika ngazi ya Wilaya,Miji mingi  watu wamezidi kuongezeka ambapo ukuaji huo unaonekana haukutiliwa mkazo wakati wa mwongozo wa awali ulio andaliwa miaka 11 iliyopita,ambapo sasa kuna kasi ya ongezeko ya ukuaji wa miji na vijiji, mwongozo huu utaangalia  namna gani mambo haya yote yataendelezwa vizuri.

Kwa upande wake Afisa Programu kutoka Haki Ardhi Bw. Joseph Chiombola ambao wanajihusisha na utafiti pamoja na utetezi wa maswala ya ardhi alisema kuwa Haki Ardhi ni jukwaa ambalo limekuwa likiendesha mijadala mbalimbali inayohusiana na maswala ya ardhi nchini Tanzania, na kwamba maswala ya matumizi ya ardhi yanahitaji mjadala mpana unaotakiwa kuwahusisha wananchi kwa ujumla.

“Moja ya malengo yetu ni pamoja na kuhakikisha kwamba kunafanyika mabadiliko ya Sera,Sheria,kanuni na miongozo mbalimbali, na hili swala la mipango na matumizi ya ardhi ni sehemu moja tunayo iangalia kwa sababu kama ikiendelezwa ipasavyo itasaidia kuweka ulinzi wa ardhi na wazalishaji wadogo ambayo ndio jukwaa tulilokuwa tukizungumzia sana kwa ajili ya haki zao kwa kipindi chote cha uwepo wetu” alisema Chiombola.

Aliongeza kuwa mipango hii ni muhimu kwa sababu inawagusa wazalishaji wa kila siku wakiwemo wakulima,wafugaji, waokota matunda,warina asali na wavuvi kwa kuwa wamekuwa wanahusika na ardhi kwa namna moja au nyengine. Hivyo mipango itakayokuwa kwa manufaa ya jamii hizo itakuwa na manufaa makubwa katika kuongeza kipato chao na kubadilisha hali ya maisha yao. 

Nae Naibu Katibu Mkuu wa wa Chama cha Wafugaji Tanzania Bw. Joshua Lugaso alisema kuwa kutengeneza urejewa mwongozo wa upangaji,utekelezaji na usimamizi wa mipango ya matumizi ya Ardhi ya Wilaya utakuwa ni mkombozi kwa mfugaji kutambulika katika maswala ya ardhi Tanzania jambo ambalo halijawahi kutokea kwa miaka mingi.

“Katika mwongozo huu mfugaji ameonekana sana na kuondoa dhana ya kila wakati wakulima kuonekana, tunaamini kwamba ni mpango unaoenda kufanya kazi  kwenye Wilaya tunaamini kwamba ikisimamiwa vizuri, migogoro ya wafugaji na wakulima itakwisha” alisema Lugaso.

Katika mwongozo  uliopita kulikuwa na mapungufu ambayo ni  pamoja na mkazo wa namna ya jamii zinavyokabiliana na mabadiliko ya Tabianchi haukuwa na mkazo mkubwa,hakukuwa na mkazo wa namna ya ardhi za Wilaya zinavyopangwa ili kuhakikisha kwamba kunakuwa kuna ukuwaji wa viwanda katika ardhi ya wilaya au ya vijiji, pia swala la ushirikishwaji katika upande wa jinsia na makundi madogo madogo wanaotumia ardhi ambao katika jamii hawana nguvu ya kisiasa,kiuchumi  kwa kuwa na wao wanatakiwa watambuliwe.

No comments:

Post a Comment

Pages