HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 20, 2017

NSSF yawafikiwa watanzania waliopo katika sekta isiyo rasmi

Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limejikita katika kuwafikia watanzania wengi zaidi ikiwa ni katika azma yake ya kuboresha maisha yao kwa kuwapatia huduma ya matibabu bure pindi watakapojiunga na mfuko huo wa jamii.


Akizungumza wakati wa kampeni ya kutoa elimu na kuandikisha wanachama walio katika sekta isiyo rasmi inayoendelea katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam Kaimu Meneja wa Masoko na Uhusiano, Salim Kimaro alibainisha hayo jijini Dar es Salaam akisema kuwa mfuko huo wa jamii umejizatiti kuandikisha na kutoa mafao yaliyo bora kabisa kwa Wanachama wake.

Kimaro ametaja baadhi ya mafao hayo kuwa ni mafao ya matibabu bure kwa mwanachama na wategemezi wao, mafao ya uzazi yanayotolewa na mfuko huo wa jamii wa NSSF.

Aidha Kimaro amewaasa watanzania kuwa na utaratibu wa kujiwekea akiba kwa ajili ya maisha yao ya baadae kwa kujiunga na NSSF.

Ofisa Mkuu Mwandamizi Kitengo cha Sekta Isiyo Rasmi kutoka Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Abas Cothem, akimwandikisha kujiunga na NSSF mwanachama mpyam, Mariam Daimon katika eneo la Makumbusho jijini Dar es Salaam jana, wakati wa zoezi la kutoa elimu juu ya uanachama wa hiari wa NSSF. (Na Mpiga Picha Wetu).

Ofisa Mkuu Mwandamizi Kitengo cha Sekta Isiyo Rasmi kutoka Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Abas Cothem, akitoa elimu juu ya uanachama wa hiari wa NSSF kwa wananchi katika eneo la Makumbusho jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki, wakati wa zoezi la kutoa elimu juu ya uanachama wa hiari wa NSSF.

No comments:

Post a Comment

Pages