HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 20, 2017

BREAKING NEWS: WAKILI DK. RINGO TENGA KIZIMBANI KWA KOSA LA UHUJUMU UCHUMI

Dar es Salaam, Tanzania, Novemba 20 

Vigogo wanne wa Kampuni ya Six Telecoms Limited wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka ya uhujumu uchumi ikiwemo kuisababishia serikali hasara ya Dola za kimarekani Milion.3.7 ambayo ni sawa na bilioni nane.

Washtakiwa hao ambao leo wamefikishwa mahakamani hapo majira ya saa tatu asubuhi na wamesomewa mashtaka yao na wakili wa Serikali, Jehovaness Zacharia mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Victoria Nongwa.

Washtakiwa katika kesi hiyo ni Mhandisi na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo, Hafidhi Shamte, aliyekuwa Mkurugenzi wa benki ya Rasilimali watu (TIB), Mfanyabiashara na pia ni Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Peter Noni, Wakili maarufu wa kujitegemea, Mhadhiri na Mkurugenzi pia wa kampuni hiyo Ringo Tenga, Mkuu wa fedha wa kampuni hiyo Noel Chacha na Kampuni ya Six Telecoms Limited.

Akisoma hati ya mashtaka katika kesi hiyo namba 73 ya 2017, Wakili Zacharias alidai kuwa kati ya Januari Mosi 2014 na Januari 14, 2016 jijini Dar es Salaam washtakiwa hao, walitoza maalipo ya Mawasiliano ya simu za kimataifa chini ya kiwango cha dola 0.25 kwa dakika kwa lengo la kujipatia faida binafsi.

Alidai kuwa katika siku hizo hizo washtakiwa kwa udanganyifu na kwania ya kuepuka malipo, walishindwa kulipa kiasi cha dola 3,282,741.12 kama mapato kwa TCRA

Vile vile washtakiwa hao wanadaiwa kushindwa kulipa ada za udhibiti za dola 466,010.07 kwa TCRA.

Katika mashtaka ya utakatishaji washtakiwa Hafidhi, Noni,Tenga na Chacha wanadaiwa kujipatia, kutumia ama walisimamia USD 3,282,741.12 wakati wakijua fedha hizo ni zao la makosa ya udanganyifu linalotokana makosa mengine wanayoshtakiwa nayo.

Aidha katika shtaka la tano, inadaiwa kuwa kampuni ya Six Telecoms ilijipatia, ilitumia na kusimamia dola 3,282,741.12 wakati ikijua fedha hizo ni zao la makosa ya udanganyifu yanayotokana Mashtaka yaliyotangulia.

Katika shtaka la mwisho, wshtakiwa wote hao waliisababishia TCRA hasara ya USD 3,748,751.22 ambayo ni sawa na bilioni nane za kitanzania.

Washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu chochote kwa sababu Mahakama ya Kisutu hiyo haina Mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi.

Baada ya kumaliza kusomwa kwa mashtaka dhidi ya washtakiwa, Wakili wa utetezi, Masumbuko Lamwai aliiomba Mahakama kukataa hati ya mashtaka dhidi ya washtakiwa na kuomba upande wa mashtaka wakaandae upya

Alidai mashtaka dhidi ya washtakiwa yameletwa haraka haraka na mashtaka hayako sawa sawa ambapo alidai
Mashtaka hayo hayaonyeshi mshtakiwa yupi katenda kosa gani na hati ya mashtaka ilitakiwa kuonyesha makosa.

Baada ya mabishano makali ya kisheria, mahakama imeahirisha kesi hiyo hadi Novemba 24, mwaka huu kwa ajili ya kutolea maamuzi dhidi ya mabishano hayo na washtakiwa wamerudishwa rumande.Wakili maarufu Dk. Ringo Tenga, aliyekuwa Mkurugenzi wa Benki ya Rasilimali Tanzania (TIB), Peter Noni, pamoja na washtakiwa wengine watatu leo wamefikishwa mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Victoria Nongwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, wakikabiliwa na kesi ya Uhujumu Uchumi. Habari kamili zitawajia hivi punde.


Wakili maarufu Dk. Ringo Tenga (mbele), aliyekuwa Mkurugenzi wa Benki ya Rasilimali Tanzania (TIB), Peter Noni (nyumba ya Dk. Ringo), wakiingia katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo Novemba 20 2017 wakikabiliwa na shtaka la Uhujumu Uchumi ikiwemo kuisababishia serikali hasara ya Dola za kimarekani Milion.3.7 ambayo ni sawa na bilioni nane..

Wakili maarufu Dk. Ringo Tenga (mbele), aliyekuwa Mkurugenzi wa Benki ya Rasilimali Tanzania (TIB), Peter Noni (nyumba ya Dk. Ringo), wakiingia katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo Novemba 20 2017 wakikabiliwa na kesi ya Uhujumu Uchumi.

Wakiwa katika chumba cha mahakama.

Washtakiwa wakiwa katika chumba cha mahakama.

Wakili maarufu Dk. Ringo Tenga (katikati), akiwa katika mahakama ya Kisutu wakati kabla ya kesi yao kuanza kusikilizwa. Kushoto ni aliyekuwa Mkurugenzi wa Benki ya Rasilimali Tanzania (TIB), Peter Noni.

No comments:

Post a Comment

Pages