Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir
Ali akitoa salamu kwenye sherehe za Baraza la Maulid ya Uzawa wa Mtume Muhammad (SAW) Mkoani Lindi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali
Iddi akilihutubia Baraza la Maulid ya Uzawa wa Mtume Muhammad (SAW) katika Viwanja vya Kijiji cha Rikangala Wilaya ya Ruangwa Mkoani
Lindi.
Lindi, Tanzania
MAKAMU wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi amewataka Waislam nchini kote kuwa waadilifu kama alivyokuwa Mtume Muhammad (S.A.W).
Ali akitoa salamu kwenye sherehe za Baraza la Maulid ya Uzawa wa Mtume Muhammad (SAW) Mkoani Lindi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali
Iddi akilihutubia Baraza la Maulid ya Uzawa wa Mtume Muhammad (SAW) katika Viwanja vya Kijiji cha Rikangala Wilaya ya Ruangwa Mkoani
Lindi.
Lindi, Tanzania
MAKAMU wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi amewataka Waislam nchini kote kuwa waadilifu kama alivyokuwa Mtume Muhammad (S.A.W).
Amesema ni vema wakatumia
wakati huu wa Maulid kutathmini mienendo ya maisha yao kwa kujiuliza kama
maisha wanayoishi yanafanana na yale
aliyoishi Mtume Muhammad.
Balozi Seif ameyasema hayo
leo (Ijumaa, Desemba Mosi, 2017) alipokuwa mgeni rasmi katika Baraza la Maulid
ya Mtume Muhammad (S.A.W) lililofanyika kitaifa wilayani Ruangwa mkoa wa Lindi.
“Kuna vigezo vingi mja
anaweza kuvitumia wakati anapojitathmini, ambavyo ni pamoja na tabia ya Bw
Mtume ya uadilifu na wake. Tujiulize
kati yetu hapa ni wangapi waadilifu na waaminifu kama alivyokuwa Bw. Mtume.”
Amesema kupungua kwa
uaminifu na uadilifu ndiko kulikomfanya Rais Dkt. John Magufuli mara baada ya
kuingia madarakani kuanzisha vita dhidi ya vitendo vya rushwa na ufisadi, hivyo
wanatakiwa kumuunga mkono.
Balozi Seif amesema Waislam
waka kila sababu ya kushirikiana na Rais Dkt. Magufuli katika mapambano hayo
kwa sababu kupinga vitendo vya rushwa na ufisadi ni ibada kwao.
“Mtume (S.A.W) aliikemea
sana rushwa na akasema kuwa amelaaniwa na Mwenyezi Mungu mwenye kutoa na
kupokea rushwa na hata Yule mpiga debe. Pia tunaamini kuwa dini zote duniani
zinapinga rushwa, hivyo tuiiepuke”
Pia amewaomba viongozi wa dini
zote nchini waendelee kushirikiana na Seikali kwa kuhubiri amani, utulivu na mshikamano ili kujenga
umoja kwa Watanzania wote. “Siku zote mmekuwa mkitusaidia sana kupitia mahubiri
yenu kwa kujenga umoja kwa Watanzania wote bila ya kujali dini zao,rangi wala
kabila. Nawaomba muendelee na moyo huo.”
Awali, Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Aboubakar
Bin Zubeiry alisema aliwaasa Watanzania wote waendelee kuidumisha na kuitunza
amani kwa sababu hakuna maendeleo yoyote yatakayopatikana bila ya kuwepo kwa
amani.
Alisema suala la kudumisha
amani, kuheshimiana na kushirikiana miongoni mwa waislamu na wasiokuwa waislam
limehimizwa sana katika dini ya kiislam na dini nyingine, hivyo wananchi hawana
budi kuendeleza.
Kwa upande wake, Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa alimpongeza Sheikh Mkuu kwa uongozi wake mzuri wa Baraza la WaislamTanzani (BAKWATA) ikiwa ni
pamoja na kufanya kazi na dini zote bila Ubaguzi.
Alisem serikali itaendelea
kufanya kazi na dini zote na kwamba Rais Dkt. Magufuli amezipa kipaumbele
shughuli za dini zote ziendelee kufanyika nchini.
Baraza hilo lilihudhuriwa na
Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Zubeiry, Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary
Majaliwa, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Bw. Suleiman Jafo, Naibu
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhandisi Stella Manyanya.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Bw. Abdallah
Ulega, Naibu Waziri wa Maji Bw. Jumaa Aweso, Naibu Waziri wa Nishati Bibi
Subira Mgalu, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri, Bibi Stellah Ikupa Alex,
Naibu Waziri wa Madini Bw. Stansilaus Nyongo na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri
Mkuu Bibi Maimuna Tarishi.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya
Wanawake wa Kiislamu Tanzania, Bibi Shamim Khan, Mkunge wa Kibiti Bw. Ally Ungando,
Mbunge wa Liwale Bw. Zubeiry Kuchauka, Mbunge wa Nachingwea Bw. Hassan Masalla,
Mbunge wa Lindi Mjini, Hassan Kaunje Mbunge wa Viti Maalumu Bibi Hamida
Abdallah.
Wengine ni Askofu Mkuu wa
Jimbo Kuu wa Jimbo Katoliki la Lindi, Bruno Ngonyani, Mkurugenzi wa Taasisi ya
Alhikma, Kiongozi Mkuu wa Kiroho wa Dhehebu la Shia Ithnasheri, masheikh wa
mikoa yote pamoja na wananchi wa Lindi pamoja na mikoa mbalimbali nchini.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
IJUMAA, DESEMBA MOSI, 2017.
No comments:
Post a Comment