Klabu ya soka ya JKT Ruvu Stars ambayo inashiriki ligi kuu Daraja la kwanza msimu wa mwaka 2018-2019 itabadilishwa jina na kuitwa JKT Tanzania Sports Club, baada ya wamiliki wa timu za majeshi kukubali kumiliki timu moja itakayowakilisha Majeshi.
Timu za majeshi zilikuwa nyingi ambapo sheria na kanuni namba 11 ya TFF inawabana wamiliki wa timu hizo kuwa na timu mbili zinazoshiriki ligi kuu Tanzania bara.
Akitoa taarifa hiyo leo, Luteni Kanali Hasani Mabena ambaye ndiye Mwenyekiti wa timu ya JKT Ruvu amesema wamepokea barua kutoka TFF tayari wameifanyia kazi na wamewaita viongozi wote wa vilabu vya jeshi kuweza kuongea suala hilo na kukubali kwamba timu moja itabakishwa itakayomilikiwa na Jeshi la JKT, nyingine zitarudi kwa wananchi.
''Ni kweli tumepokea taarifa hiyo tumeshakaa vikao tumeamua kuibadilisha jina, JKT Ruvu na itakuwa JKT Tanzania Sports Club, ni timu pekee inayobakia kuwa timu inayomilikiwa na Jeshi, zilizobaki zitaelekezwa kwa wananchi au zitakuwa kampuni kama ilivyofanya Ruvu Shooting ,'' amesema.
Timu hizo ni pamoja na JKT Mlale, Mgambo JKT na Ruvu Shooting, wakati Ruvu Shooting imeshajiondoa katika umiliki wa Jeshi hilo na kubakia kampuni.

No comments:
Post a Comment