John Pombe Magufuli ameitaka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), kuwakamata wale wote wanaosambaza takwimu mbalimbali zinazopingana na zinazotolewa na ofisi ya takwimu ya taifa.
Magufuli amesema hayo alipokuwa akiweka jiwe la msingi katika jengo la ofisi ya Taifa ya Takwimu Dodoma na kuwataka wananchi kuwa makini na masuala ya takwimu pia amewataka kuwapuuza watu ambao wanasema vyuma vimekaza ili hala watu wa Takwimu wanasema vyuma vimefunguka.
"Ukikosea kutoa takwimu umeichafua nchi, takwimu ni kitu kibaya sana ndiyo maana kuna watu wamebobea kwenye takwimu hivyo wananchi tuwasikilize watu wa takwimu asitokee mtu mwingine akatoa takwimu tofauti na zile walizonazo watu wa takwimu. Mtu anasema vyuma vimekaza wakati watu wa takwimu wanasema vyuma vimefunguka watu hawa wanatakiwa kukamatwa na kuwekwa ndani ili wakajifunze kutoa takwimu huko" alisema Rais Magufuli
Mbali na hilo Rais Magufuli ameagiza watu ambao watatoa taarifa zozote ambazo zipo kinyume na takwimu walizonazo watu wa takwimu wafikishwe mahakamani "Mimi ningekuwa hakimu watu wa namna hiyo wangepewa adhabu zote mbili kulipa faini na kufungwa.
"Dk Chua ukisikia mtu anatoa takwimu za uongo usisubiri mkamateni nafikishwe mahakamani"
Mbali na hilo Magufuli amewataka wananchi na taasisi mbalimbali wakitaka takwimu yoyote ile waende ofisi ya Takwimu na wasithubutu kutoa takwimu ambazo zinapingana na zile zilizopo ofisi ya takwimu.

No comments:
Post a Comment